Kusudi la maisha, ni kile kitu ambacho mtu umeletwa kufanya hapa duniani. Ni kile pekee ambacho kinatofautisha maisha yako na ya wengine. Kila mtu ana kusudi lake, na hakuna makusudi yanayofanana kwa kila kitu.

Maono ni pale akili inachoona kisichokuwepo na kuwa na imani kwamba kitakuwepo. Maono ni kitu ambacho kwa uhalisia bado hakipo, ila kwa imani, kinakuwa na uhakika wa kuwepo.

Kila Mmoja

Sasa, watu pekee wanaoishi maisha yao hapa duniani, ni wale ambao wanaliona kusudi la maisha yao. Yaani watu hawa wanajua wapo hapa duniani kufanya nini, na pia wanajiona tayari wanafanya kile walicholetwa kufanya hapa duniani, hata kama kwa sasa bado hawajaanza kufanya.

SOMA; UKURASA WA 858; Kuona Unachotaka Kuona…

Kuona kusudi ndiyo njia pekee ya kushinda changamoto za maisha na ugumu wa njia ya kufika kwenye kusudi la maisha yetu. Wakati wengine wanakuambia ni ngumu na haiwezekani, wewe huwaelewi, kwa sababu ndani yako unajiona kabisa upo pale unapotaka kuwa, hata kama bado hujafika.

Ni aina hii ya imani, ambayo inaweza kufanya makubwa kuliko wengine wanavyoweza kufikiri.

Kuwa na maono ya kusudi la maisha yako na ishi maono hayo kila siku, hii ndiyo njia ya kufikia yale maisha ambayo mtu unayataka.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog