“Hold every hour in your grasp. Lay hold of to-day’s task, and you will not need to depend so much upon to-morrow’s. While we are postponing, life speeds by.” – Seneca.

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuishi kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari WAKATI UNAAHIRISHA, MAISHA YANAKUPITA…
Huwa ni rahisi kwetu kuahirisha yale ambayo mtu umepanga kufanya, ukiona baadaye au kesho utapata muda zaidi wa kufanya.
Tunachosahau ni kwamba, muda huu ambao tulikuwa tumepanga tufanye, halafu tukaahirisha, ni muda ambao tumechagua kuupoteza.

Maana muda huo hatutautumia kufanya kingine kikubwa, na tutaona ni muda mdogo kuweza kupanga kitu kingine kwa wakati huo.
Ndiyo maana kwa lolote unaloahirisha, maisha yanakupita.

Maisha yanakupita kwa sababu dunia haikusubiri mpaka wewe uwe tayari, dunia inaendelea na yake.
Na pia muda uliopanga ufanye kitu na sasa umeahirisha, ni muda unaopoteza.

Ipe kila dakika na saa yako heshima inayostahili,
Fanya kila ulichopanga kufanya hata kama kumetokea nini.
Kila unapojishawishi kuahirisha kile ulichopanga kufanya jikumbushe kwamba dunia haikusubiri wewe uwe tayari, yenyewe inaendelea kwenda.

Muda ulionao ni mfupi na una thamani kubwa sana.
Usiupoteze hovyo kwa kuahirisha yale uliyopanga kufanya.

Uwe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha