“Nothing is worth more than this day.” —JOHANN WOLFGANG VON GOETHE
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA na mwongozo wetu ni TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari HAKUNA SIKU MUHIMU KAMA LEO…
Leo ni siku muhimu sana kwenye maisha yako,
Ni siku muhimu kwa sababu unayo nafasi ya kwenda kuchukua hatua kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Unaweza kutumia muda wa leo kufanya yale yaliyo bora kabisa.
Leo ndiyo siku unayokwenda kufanya yale uliyoahirisha jana.
Leo ndiyo siku ambayo utafanya yale unayotaka kujiambia utafanya kesho.
Leo ni muhimu sana kwa sababu muda wa leo unao, upo mikononi mwako.
Jana imeshapita, huwezi kubadili cha jana.
Kesho bado haijafika, hivyo huwezi kuiathiri kwa vyovyote.
Lakini leo, leo unaweza kufanya chochote kwenye maisha yako.
Leo unaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
Usikibali kuipoteza siku hii ya leo, maana ni siku muhimu sana na haiyojirudia tena.
Uwe na siku bora sana leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha