Kila wakati jifunze kuzikubali changamoto kwenye maisha yako na changamoto hizo zitakukomaza na zitakusaidia kukua kimafanikio. Kila changamoto utakayojifunza nayo itakupa fundisho ambalo litakukuza kimafanikio.
Jifunze kuweka juhudi kila siku kwa kile unachokifanya. Kwa kuweka juhudi hizo kutakufanya wewe kuwa imara na hodari kwa hicho ukifacho. Juhudi zozote unazoziweka haziwezi kukuacha patupu lazima zikutolee matunda.
Jifunze kutoa mchango chanya kwenye maisha yako na ya wengine. Kwa mchango huo unaoutoa kila wakati, utapelekea maisha yako kuzidi kuwa ya kimafabnnikio sana.hapa kwa kifupi utavuna kile ambacho unakipanda kwenye maisha yako.
Jifunze kuzungukwa na watu ambao wana mitazamo na mawazo chanya. Kwa kuzungukwa na watu hao itakusaidia sana wewe kuweza kujifunza mengi sana. Ni wazi kabisa unapokuwa na watu wenye mawazo mazuri utajifunza mengi kwao pia.
Jifunze kugundua kitu chochote ambacho ulikuwa hujajifunza. Kwa kujifunza kitu hicho utatanua sana maarifa yako na maarifa hayo yatakusaidia kwenye mafanikio yako. Siku zote maarifa yanakuwa yana nguvu sana ikiwa lakini kama utayatumia.
Jifunze pia kwenye maisha yako kusikiliza. Kila unapokuwa unasikiliza itakusaidia kuendelea kuwa mtu wa busara kwa sababu ya usikilizaji huo. Kwa kawaida kama huna tabia ya kusikiliza, si rahisi kuweza kuelewa na utakosa busara tu.
Jifunze kutoa na maisha yako yatatawaliwa na baraka kubwa sana. Watu wengi ambao wanakua ni watu wa kutoa, kiuhalisia ni watu ambao wanatengeneza muujiza mkubwa wa maisha yao kwa kuvuta mafanikio mengine zaidi.
Jifunze kuwa ni mtu wa shukrani.. kila unapokuwa mtu wa shukrani ukumbuke unaongeza thamani kwenye kile unachokishukuru, lakini pia unaongeza thamani kwenye maisha yako kwa ujumla kwa sababu utapata zaidi na zaidi.
Jifunze kutumia wakati ulionao sasa vizuri. Wakati huu wa sasa ukiutumia vizuri utakupa matokeo bora na chanya kwa ajili ya kesho. Usiwe mtu wa kusema nitafanya hili kesho au wakati mwingine, ujue hauna uhakika wa kesho hiyo.
Jifunze kupenda kitu fulani leo, kitu hicho kipe pendo lote. Na katika kupenda huko itakusaidia kufanya kitu au kushirikiana na hicho kwa ukamilifu zaidi pengine hata kuliko ambavyo ungeweza kukichukia kitu hicho.
Elewa unapopenda na kuelewa mambo haya, unakuwa unajiweka kwenye wakati mzuri wa kukuza busara na mafanikio makubwa kwako. Jitahidi kila unachokifanya jifunze na kukipenda kitu hicho kwenye maisha yako.
Watu wenye mafanikio wanajua jinsi ya kujifunza kupitia changamoto, juhudi, na hata kujifunza juu ya watu wengine na hali ambayo inawapa mafanikio makubwa sana maishani mwao na zoezi hili wanalifanya mara kwa mara.
Hata wewe ili kufanikiwa unatakiwa kujifunza juu ya mambo hayo. Huhitaji kusubiri bali unatakiwa kuanza sasa. Kumbuka, ukijifunza kupenda na kuyaelewa mambo haya uwe na uhakika yatakusaidia sana kuweza kufanikiwa kwa namna moja au nyingine.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Tovuti; http//www.amkamtanzania.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com