Hivi ni vitu vitatu vyenye nguvu kubwa ya kufanya maisha yako yawe ya mafanikio au ya kushindwa.

Tumaini ni nguvu inayokusukuma kupiga hatua zaidi, hata kama huoni kile unachokwenda kupata na wala huna uhakika nacho. Tumaini linakufanya uamini usichokiona na uwe na uhakika wa kukipata, hata kama hujawahi kukipata huko nyuma. Tumaini ndiyo nguvu inayokufanya uendelee kupiga hatua hata baada ya kuanguka na kushindwa. Unapokuwa na tumaini, unakuwa na nguvu ya kupiga hatua. Unapokosa tumaini, unashindwa kabla hata ya kuanza. Hakikisha mara zote unakuwa na tumaini, linalokusukuma kuchukua hatua zaidi.

Mtu pekee

Hofu ni nguvu inayokuzuia usichukue hatua. Ni nguvu inayokuonesha mabaya, inayokufanya uone hatua unayochukua ni hatua mbaya na yenye matokeo mabaya. Hofu inaondoa kila aina ya hamasa ambayo mtu anakuwa nayo. Wakati mwingine hofu haiji kama hofu, badala yake inakuja kama sababu za kuahirisha. Ili kupiga hatua, lazima uweze kuishinda hofu na siyo kutokuwa na hofu kabisa. Ione hofu inapokujia, kisha ishinde kwa kuchukua hatua licha ya kuwa na hofu.

SOMA; UKURASA WA 1111; Tofauti Ya Washindi Na Wanaoshindwa Kwenye Ndoto…

Ndoto ni nguvu inayokupa sababu ya kuchukua hatua. Kile unachokiona kwenye taswira ya akili yako, japokuwa siyo halisi kwa wakati huo, ndiyo kinafanya tumaini lifanye kazi na hofu ishindwe. Ni ndoto kubwa ndiyo zinawasukuma watu kuchukua hatua kubwa zaidi. Ukiwa na ndoto kubwa unakuwa na msukumo mkubwa, ukiwa na ndoto ndogo unakuwa na msukumo mdogo.

Kumbuka nguvu hizi tatu; TUMAINI, HOFU NA NDOTO na zitumie vizuri kwa mafanikio yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog