“All life is an experiment. The more experiments you make, the better.” — Ralph Waldo Emerson

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari FANYA MAJARIBIO MENGI ZAIDI…
Ni jambo la kushangaza pale mtu anapofanya kitu mara moja, au mara chache, hapati alichokuwa anataka, halafu anajiambia kwamba ameshindwa au haiwezekani!!
Hivi unajua unapaswa kujaribu mara ngapi mpaka useme kwamba umeshindwa au haiwezekani?
Thomas Edison alijaribu kutengeneza taa ya umeme kwa zaidi ya mara elfu kumi, na ndiyo akafanikiwa kuitengeneza.
Sasa iweje wewe mara moja, au mara tatu unasema haiwzekani au umeahindwa?

Maisha ni majaribio, na kadiri unavyojaribu mambo mengi zaidi, ndivyo unavyokuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa.
Kadiri unavyoendelea kujaribu hata baada ya kukosa, ndivyo unavyoendelea kujifunza na kuwa bora zaidi.

Kamwe usijiambie umeahindwa au haiwezekani kwa sababu imejaribu mara moja, au hata mara kumi na hukupata ulichotegemea kupata.
Jaribu mara nyingi uwezavyo,
Weka juhudi kila wakati,
Na kama hutakata tamaa, basi utapata kile unachotaka.

Kadiri unavyojaribu mengi zaidi, ndivyo unavyokuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kujaribu mengi zaidi.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha