Rafiki yangu mpendwa,

Kwa siku kadhaa zilizopita nimekuwa nakupa taarifa kuhusiana na semina ya ukuaji wa biashara na kuongeza faida kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Hii ni semina muhimu sana ya kibiashara niliyoiandaa kwa mwaka huu 2018, ambayo mtu yeyote aliyepo kwenye biashara au anatarajia kuingia kwenye biashara anapaswa kushiriki.

Kupitia semina hii, tunakwenda kujifunza msingi muhimu sana wa ukuaji wa biashara na kuongeza faida kwa kiasi kikubwa, kwa kuzingatia maeneo matano muhimu sana ya biashara zetu.

Tutakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo mtu ukiweza kuzitumia, biashara yako lazima itapiga hatua, utakuwa na wateja wengi zaidi, utauza zaidi na utatengeneza faida zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao wa wasap, kupitia kundi la KISIMA CHA MAARIFA, na itaanza tarehe 05/07/2018 na itafanyika kwa siku 7 mfululizo. Mwisho wa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili kuweza kushiriki semina hii itakuwa tarehe 03/07/2018.

Rafiki, nimeshakueleza mengi kuhusu KISIMA CHA MAARIFA na hata semina hii, lakini bado wapo ambao wanauliza maswali mbalimbali. Kwenye makala hii nimekusanya yale maswali ambayo yanaulizwa sana na kukupa majibu yake, ili kwa wale ambao bado wana maswali na hawajapata nafasi ya kuyauliza basi wapate majibu na kuweza kuchukua hatua sahihi.

Msingi Mkuu

Yafuatayo ni maswali na majibu ambayo yanaulizwa sana na wengi kuhusiana na KISIMA CHA MAARIFA na semina ya ukuaji wa biashara.

Swali; KISIMA CHA MAARIFA ni nini?

Jibu; KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya mafunzo ya mafanikio kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla. Kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, unapata nafasi ya kusoma makala kwenye mtandao wa KISIMA ambazo ni makala kwa ajili ya wanachama pekee. Pia unapata nafasi ya kuingia kwenye kundi maalumu la Wasap ambapo kila siku unapata mafunzo na hamasa ya kuweza kupiga hatua zaidi.

Swali; ukiacha mafunzo ya kila siku, zipi faida nyingine za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Jibu; kuna faida lukuki ukiacha mafunzo ya kila siku. Kuna madarasa ya kila wiki ambapo unajifunza mada mbalimbali, kuanzia biashara mpaka afya, falsafa mpaka kujijengea tabia binafsi. Pia kila mwaka unashiriki semina tatu, mbili kwa njia ya mtandao na moja ya kukutana ana kwa ana. Na faida nyingine kubwa ya kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, unapata nafasi ya kufanya kazi kwa karibu na Kocha Makirita kwenye programu ya PERSONAL COACHING ambapo kocha anafanya kazi na wewe kwa karibu ili kufikia malengo uliyojiwekea.

Swali; unajiungaje na KISIMA CHA MAARIFA.

Jibu; kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, unalipa ada ya mwaka, ambayo kwa sasa ni tsh 50,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha unatuma ujumbe kwa njia ya wasap, namba 0717396253 wenye majina yako kamili, namba ya simu na email yako. Hapo utapewa maelekezo ya kujiunga na kuwekwa kwenye kundi la wasap.

Swali; je siwezi kulipa ada kidogo kidogo?

Jibu; hapana, hakuna mpango wa kulipa ada kidogo kidogo. Ada inapaswa kulipa yote kamili na uweze kupata masomo kwa mwaka mzima bila ya usumbufu wowote. Lakini pia natoa nafasi chache sana kwa wale ambao wanaweza kulipa kwa awamu mbili, kulipa nusu kwanza na nusu iliyobaki kulipwa ndani ya mwezi mmoja. Kama kweli huwezi kulipa ada kamili, tuwasiliane na nitakupa mpango huo wa kulipa kwa awamu mbili. Muhimu; kabla hujalipia nusu tuwasiliane kwanza ili nikuambie kama nafasi hiyo bado ipo, maana nafasi hizo ni chache.

Swali; siwezi kushiriki semina hiyo, maana nipo mbali na kazi zimenibana.

Jibu; semina hii haikutaki wewe usafiri kwenda popote. Semina inaendeshwa kwa njia ya mtandao na unaweza kushiriki ukiwa popote. Pia huhitaji kutenga siku yako kwa ajili ya semina. Unahitaji kutenga angalau nusu saa tu kwenye siku yako kufuatilia mafunzo ya semina na kupanga hatua za kuchukua.

Swali; huwa sipati muda wa kuingia kwenye makundi ya wasap, nina mambo mengi.

Jibu; kundi la KISIMA CHA MAARIFA ni kundi la wasap la kipekee, sana, nakuambia hujawahi kuwa kwenye kundi kama hili kwenye maisha yako yote. hakuna ujumbe, mapicha na mavideo ya kijinga utakayokutana nayo kwenye kundi hili. Hutakutana na habari yoyote ile, hata iwe ya kusisimua kiasi gani. Ndani yake ni maarifa mwanzo mwisho, na jumbe ni chache lakini zenye maana kubwa. Hivyo ukitenga nusu saa yako kwa siku ya kujifunza, inakutosha kabisa. Na kama kwa siku huna nusu saa ya kujifunza, basi huna maisha, na unahitaji kuchukua hatua mara moja juu ya maisha yako.

Swali; semina inaweza kuendeshwaje kwa njia ya mtandao? Sijawahi kuona hilo?

Jibu; karibu sasa ujiunge na utaona jinsi mtandao unavyorahisisha mafunzo. Semina inaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, kila siku asubuhi unapata somo la semina, lenye mafunzo na hatua za wewe kuchukua, ambazo utahitaji kuziandika chini kabisa. Kisha kama una swali au chochote unachohitaji ufafanuzi unaweza kuuliza na utapata majibu moja kwa moja kutoka kwa kocha. Yaani unapata kila kitu unachoweza kupata kwenye semina yoyote ile, sema tu huna haja ya kusafiri na kuacha shughuli zako nyingine.

Swali; vipi kama nikilipa halafu sijayapenda mafunzo ninayopata.

Jibu; naelewa hakuna kitu ambacho kinamfaa kila mtu, hata kama kitu ni kizuri kiasi gani, kuna watu hakitawafaa. Hivyo unaweza kujaribu, ukiona aina ya mafunzo unayopata siyo uliyotegemea, unaniambia mafunzo hayakufai na sitakuuliza swali la ziada zaidi ya kukurudishia ada uliyolipa. Na kama utaona yanakufaa, na ukakaa mwaka mzima, ukijifunza na kuchukua hatua, lakini baada ya mwaka maisha yako yakabaki vile vile, usione mabadiliko yoyote ndani yako, basi unaniambia na ninakurudishia mara mbili ya ada uliyolipa.

Swali; mimi semina za mtandaoni siziwezi, nataka ya kuhudhuria moja kwa moja.

Jibu; usijali, hiyo ya kuhudhuria moja kwa moja inakuja mwezi oktoba. Lakini ili uweze kushiriki semina hiyo ya kuhudhuria moja kwa moja, lazima uwe mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, Hivyo karibu ujiunge sasa ili usikose nafasi ya kushiriki semina ya kuhudhuria moja kwa moja.

Swali; napenda sana kushiriki semina hii lakini sina fedha, mambo yamebana kweli.

Jibu; sababu kwamba huna fedha ya kuweza kulipia na kupata mafunzo haya, ndiyo inapaswa kuwa msukumo kwako kufanya lolote uwezalo, ili uweze kushiriki semina hii. Maana utapata maarifa ambayo yatakuwezesha kuongeza kipato chako, na hutahitaji kujidhalilisha tena mbele ya watu ukilalamika huna fedha na mambo ni magumu. Omba fedha, kusanya michango, uza ulivyonavyo ambavyo siyo muhimu sana na pata ada ya kushiriki semina hii, ni hatua ya msingi sana utakuwa umefanya kwenye maisha yako, na utajishukuru sana baadaye.

Swali; nimeshajifunza mengi sana kuhusu biashara, kuna jipya gani nitapata kwenye semina hiyo?

Jibu; kila mtu kuna kitu anaweza kujifunza cha kumfanya awe bora zaidi, haijalishi anajua kiasi gani. Na swala siyo tu kujifunza na kujua. Kwa mfano mengi ambayo utajifunza kwenye semina hii, tayari unayajua. Kitu ambacho semina hii itakusaidia sana ni kuchukua hatua, kuwa na mkakati ambao unaufanyia kazi, na unaweza kupima matokeo yake. Kwenye semina hii, ni kama unaondoka na kanuni ambayo unaifanyia kazi mara moja na unaona matokeo yake.

Rafiki yangu, hayo ni maswali ambayo wengi wamekuwa wanauliza na hata kujiuliza wao wenyewe. Hapo nimekupa majibu ya maswali hayo. Kama una swali ambalo hakuna jibu lake hapo, unaweza kuuliza kwa kujibu email hii au kutuma swali lako kwenye email maarifa@kisimachamaarifa.co.tz

Vinginevyo, jiunge leo na KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kupata mafunzo ya semina hii muhimu ya kukuza biashara yako.

Kama hujapata taarifa kamili kuhusu semina hii, taarifa iko hapo chini;

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha