“If you don’t ask, the answer’s always no” – Pat Croce
Siku mpya, siku bora na siku ya kipekee saa kwetu.
Tumepata nafasi nyingine nzuri sana kwetu ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata mtokeo bora sana.
Siku hii ya leo, ndiyo siku tunakwenda kuweka alama mpya kabisa kwenye maisha yetu.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JIBU NI HAPANA…
Kama hutauliza, kama hutaomba, jibu ni hapana.
Watu wengi kuna vitu huwa wanavihitaji kutoka kwa wengine, ila huwa hawasemi au kuuliza, na kinachotokea ni kwamba, hawapati kile wanachotaka.
Wengi huogopa kusema, kuomba au kuuliza kwa sababu wanahofia watakataliwa na hivyo hawatapata wanachotaka.
Cha kushangaza ni kwamba, hawaelewi hata wasiposema, kuuliza au kuomba, bado hawapati wanachotaka.
Wanachokuwa wamefanya ni kujiambia wao wenyewe hapana kabla hata hawajaambiwa na wale waliotaka kuwauliza.
Rafiki, kama hutauliza au kuomba kile unachotaka, jibu ni hapana, kwa maana hutakipata.
Lakini unapouliza au kuomba, unaongeza nafasi za majibu, jibu linaweza kuwa ndiyo au likawa hapana.
Usikubali kabisa kujiambia hapana wewe mwenyewe, uliza na omba mpaka uipate hapana kutoka kwa mhusika mwenyewe.
Na hata atakaposema hapana, huo siyo mwisho, jua kwamba njia uliyotumia siyo sahihi kwake hivyo tafuta njia nyingine.
Kila mtu ana kitu anaweza kusema ndiyo, kila mtu ana eneo lake la kusema ndiyo, unachohitaji ni wewe kuuliza na kuomba kwa njia sahihi mpaka utakapopata unachotaka.
Usipouliza jibu litabaki ni hapana,
Na usipofanya jibu litabaki ni haiwezekani.
Kama kuna kitu unataka kutoka kwa wengine, jua nani mwenye nacho kisha uliza au omba na usirudi nyuma mpaka upate kile unachotaka.
Usijiambie mwenyewe hapana, usijiambie mwenyewe haiwezekani halafu ukaridhika na kusonga mbele.
Kama ni hapana, isikie kutoka kwa mhusika na usikubali ikawa hapana kweli.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuuliza, siku ya kuomba na siku ya kufanya. Usijipe hapana, usijiambie haiwezekani.
#Fanya #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha
asante kwa kazi hizi zinazotufanya tuzidi kuwa bora katika misha yetu kocha.
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike