“To be yourself in a world that is constantly trying to make you something else is the greatest accomplishment.” — Ralph Waldo Emerson

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USHINDI MKUU NI KUWA WEWE…
Changamoto kubwa ya maisha ya hapa duniani ni kwamba kila mtu anakazana kukushawishi uwe anavyotaka yeye.
Watu watakuambia unapaswa ufanye hichi au kile ili uwe kama wao, au ndiyo uonekane una maisha bora na ya mafanikio.

Ukishawishika na maelekezo hayo ya wengine, na ukayafanya maisha yako watakavyo wao, wanaweza kukukubali, lakini ndani yako bado utajisikia kuna utupu fulani ambao utakusumbua maisha yako yote.

Kama upo kwenye ajira kwa sababu ndiyo watu wanategemea uwe hivyo,
Kama unafanya biashara kwa sababu ndiyo watu wanakuelewa kwa biashara hiyo unayofanya.
Kwa nje watu wanaweza kukubaliana na wewe, lakini kuna mtu ndani yako, ambaye unakaa naye masaa 24 hatakubaliana na wewe, na atakusumbua sana.

Mafanikio makubwa kwenye maisha yako, na ushindi mkuu kwenye maisha ni kuwa wewe.
Kuweza kuwa wewe kwenye dunia inayokulazimisha uwe kitu fulani tofauti, ni ushindi mkubwa sana.

Asubuhi hii tafakari kwenye kila eneo la maisha yako na uone kama unaishi kila eneo la maisha yako kwa kuwa ndivyo unavyotaka au unaishi hivyo ili kuwaridhisha wengine?
Kama ndiyo maisha uliyochagua, endelea kuweka juhudi.
Kama ni kwa sababu ya wengine, ni wakati wa kukaa na kupanga upya, maana kuongeza mwendo wakati umepotea njia ni kuzidi kupotea zaidi.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kuwa wewe, kufanya yaliyo muhimu kwako.

#KuwaWewe #Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha