Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NITAANZA VIZURI KESHO…
Watu huwa wanapanga vizuri sana kuhusu kuanza kufanya kitu fulani,
Wanajiambia kabisa kwamba wataanzaje na wataanzia wapi.
Inapofika wakati wa kuanza, wanapokutana na changamoti ndogo au kushindwa kidogo, wanaacha na kujiambia wataanza vizuri kesho yake.

Nitaanza vizuri kesho ni njia rahisi inayotumiwa na wengi kutoroka kuweka kazi, ni njia inayoficha uzembe na uvivu uliopo ndani ya wengi.
Ni rahisi kujiambia utaanza vizuri kesho, na kwa kuwa kesho huwa haifiki, basi hupati nafasi ya kukabili uzembe wako.

Anza leo na kama kuna kikwazo chochote kitatule leo leo na endelea kufanya.
Usifike kwenye ugumu na kusema utaanza vizuri kesho. Tatua ugumu uliokutana nao leo ili kesho uendelee vizuri.

Fanya kile ulichopanga kufanya leo, na unapokutana na ugumu ukajiambia utaanza vizuri kesho, jikamate na ona uzembe unaotaka kufanya. Kisha komaa hapo hapo mpaka uvuke ugumu huo.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuanza vizuri leo na siyo kesho.
#Fanya #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha