Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NI HATUA UNAZOCHUKUA…
Kitakachokutofautisha wewe na wengine siyo mipango uliyonayo, siyo ndoto kubwa ulizojiwekea, bali hatua unazochukua.
Kitakachokufanya ujulikane kwa wengine siyo jina lako, au maneno yako, bali hatua unazochukua.
Kitakachokutoa hapo ulipo sasa na kwenda mbele zaidi, siyo kile unachotamani, siyo mipango mizuri uliyonayo wala huruma za wengine, bali ni hayua unazochukua.
Kitakachokuwezesha kufanikiwa sana licha ya kuanzia chini siyo sababu unazojipa, wala wale unaowalaumu, bali ni hatua unazochukua.
Mengine yote unayopanga, kusema na kutamani yanabeba asilimia 1 ya mafanikio yako.
Asilimia 99 inabebwa na hatua unazochukua.
Hivyo hata ungepanga na kufurahia mipango yako kiasi gani, kama huchukui hatua unajidanganya tu, unajipa faraja zisizo na maana.
Ukishaamua nini unataka, punguza milolongo inayokuzuia wewe usifanye, na weka juhudi kubwa kwenye ufanyaji.
Hatua unazochukua ndiyo zinaleta tofauti kwako na hata kwa wengine.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchukua hatua kubwa, siku ya kuondokana na sababu za kutokuchukua hatua.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha