Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UNACHOPIGANA NACHO KINA NGUVU JUU YAKO…
Chochote unachopigana nacho, unakipa nguvu ya kukutawala wewe, u akifanya kiwe juu yako.
Chochote unachokichukia unakipa nguvu ya kukutawala, kuzifanya fikra na hisia zako ziendane na kitu hicho.
Chochote unachong’ang’ana ili kukipata, kinakutawala wewe kwenye kila eneo la maisha yako.
Kwa kujua hili, unahitaji kuwa makini sana ni wapi unaweka nguvu za maisha yako,
Usikubali vitu vidogo vidogo, visivyochangia kule unakokwenda vikutawale wewe.
Njia pekee ya kunyima kitu chochote nguvu juu yako ni kupuuza na kuachilia.
Kama kuna kitu hukipendi kwenye maisha yako, badala ya kukiwekea chuki kipuuze, na hakitakusumbua tena.
Kama kuna hali fulani inayokukwaza achilia, kubaliana nayo na acha mambo yaende kama yanavyoenda na hilo halitakutawala.
Usikubali kusumbuka na kutawaliwa na mambo madogo madogo, mambo yasiyo na maana kubwa kwako na yasiyochangia wewe kufikia ndoto zako.
Puuza na achilia, ni njia ya uhakika itakayokupa uhuru kwenye mambo mengi.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kupuuza na kuachilia yale yote ambayo hayana umuhimu mkubwa kwako. Na usikubali kutawaliwa na chochote kisichokuwa na manufaa makubwa kwako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha