Rafiki yangu mpendwa,

Salamu zangu za mafanikio zikufikie popote pale ulipo sasa, wakati unaendelea na mapambano ya kuyaboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa. Kumbuka nipo na wewe kwenye safari hii, kila wakati nikikushirikisha maarifa bora sana kwako ili uweze kufika kule unakotaka. Kwa sababu kama ambavyo nimekuwa nakusisitizia, hakuna kinachoweza kukuzuia kufanikiwa ila wewe mwenyewe.

Rafiki, katika kuuanza mwaka 2019, nimekuandalia semina ya kipekee sana, semina ambayo inakwenda kuyabadili kabisa maisha yako. Hii ni semina ambayo inakuja kujenga msingi mpya wa mafanikio na utajiri kwenye maisha yako. Semina hii inaitwa TABIA ZA KITAJIRI; Ahadi Kumi Za Kuishi Kila Siku Ili Kufikia Utajiri Na Mafanikio Makubwa Kwenye Maisha. Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo unaweza kushiriki popote ulipo bila ya kuacha shughuli zako.

elfu moja

Nimeiandaa semina hii kama zawadi ya kipekee kwa kila rafiki yangu ambaye anafuatilia mafunzo ninayoshirikisha kila siku. Nimefanya utafiti na kuja na tabia kumi ambazo kila mtu anaweza kuzifanyia kazi kila siku na maisha yake yakawa bora sana.

Na ili kuhakikisha hakuna anayekosa semina hii (labda atake mwenyewe) nimetoa njia mbili za kushiriki semina hii. Njia ya kwanza ni kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na kulipa ada ya shilingi laki moja. Lakini najua siyo kila mtu anaweza kulipa laki moja, hivyo nikaweka njia ya pili ambapo mtu analipia elfu ishirini na kuweza kupata mafunzo ya semina hii.

Sasa pamoja na kutoa nafasi hii bora na ya kipekee kwa kila mtu kuweza kushiriki, rafiki na msomaji mwenzetu aliniandikia ombi lifuatalo kwenye email; “naomba unishirikishe tabia tatu tu kwa shilingi elfu tano.”

Japokuwa hakusema kwa nini alitaka tabia tatu kwa shilingi elfu tano, iko wazi kwamba rafiki yetu huyu, elfu 20 imekuwa nyingi kwake. Na ili kuona asikose kabisa, anaona ni vyema aombe tabia zinazoendana na kile kiwango anachoweza kulipia.

Sasa kwenye haya mafunzo, hatupimi kama mtu unavyonunua mchele, kwamba kama huwezi kununua kilo moja, basi unaweza kulipia nusu kilo. Mafunzo unayafaidi pale unaposhiriki yote, maana kila kilichopo kwenye mafunzo kinategemeana na vingine.

Kwa mfano kwenye semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI, tabia zote kumi zinategemeana, kutekeleza hata tabia nane na ukaacha mbili, hutapata matokeo makubwa unayotazamia kupata. Hivyo unapaswa kushiriki mafunzo yote kamili.

Lakini kama unavyonijua mimi rafiki yako, nipo kwa ajili yako, na ombi la mwenzetu lilinifanya nifikirie mtu kama huyu, na ninajua wapo wengi, anawezaje kushiriki mafunzo haya muhimu sana kwa maisha yake?

Na hapa ndipo nilipofikiri kwa kina na kuja na jibu, na jibu lenyewe ni hili, KWA SHILINGI ELFU MOJA KILA SIKU, KWA SIKU 20, kila mtu anaweza kushiriki semina hii.

Nielezee kwa ufupi jinsi unavyoweza kushiriki semina hii kwa SHILINGI ELFU MOJA.

Kwa wale ambao siyo wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, ada ya kushiriki semina hii ni shilingi elfu 20. Mwisho wa kulipa ada hii ni tarehe 02/01/2019, hii ina maana kuna siku zaidi ya 20 za kulipa ada hiyo.

Sasa kama huwezi kupata ada hiyo kwa wakati mmoja, nakupa nafasi ya kulipia shilingi elfu moja kila siku. Unachofanya, unanitumia ujumbe kwenye namba 0717396253 na kunieleza kwamba kila siku utalipia elfu moja. Na nitatunza kumbukumbu zako. Kila siku unatuma shilingi elfu moja kwa namba 0717396253 au 0755953887 ili mpaka inapofika tarehe ya mwisho ya kulipia semina uwe umeshakamilisha kulipa.

Lakini pia unaweza kulipa mara moja yote, kulipa nusu kwa awamu mbili au kulipa robo kwa awamu nne. Rafiki yangu, nakupa kila nafasi ya kuhakikisha hukosi fursa hii ya kujijengea tabia kumi zitakazokutoa hapo ulipo sasa na kukupeleka mbele zaidi.

Swali ambalo wengi mnaweza kuwa nalo ni napata wapi shilingi elfu moja kila siku?

Na jibu lipo wazi, kwenye maisha yako ya kila siku, kuna maeneo mengi sana unayoweza kuokoa au kupata shilingi elfu moja kila siku.

Hapa nakuorodheshea machache.

  1. Acha kunywa soda kila siku na utaokoa elfu moja.
  2. Acha kununua maji na beba maji kwenye chupa yako mwenyewe na utaokoa shilingi elfu moja.
  3. Acha kununua muda wa maongezi kila siku na utaokoa zaidi ya elfu moja.
  4. Acha kununua kilevi chochote unachotumia, iwe ni pombe au sigara na utaokoa shilingi elfu moja.
  5. Acha kulipia pikipiki kwa umbali ambao ungeweza kutembea na utaokoa shilingi elfu moja.
  6. Acha kulipia ving’amuzi vya tv na utaokoa zaidi ya elfu moja.
  7. Acha kununua magazeti na utaokoa zaidi ya elfu moja.
  8. Acha kucheza michezo ya bahati nasibu na kamari na utaokoa zaidi ya elfu moja.
  9. Acha kununua vitu unavyokutana navyo, ambavyo hukupanga kununua na utaokoa zaidi ya elfu moja.
  10. Acha kufanya miamala mingi ya fedha, mfano kutoa fedha benki, kupeleka kwenye mpesa au tigo pesa kisha kutoa kwa wakala, utaokoa zaidi ya elfu moja.

Rafiki, haya ni maeneo kumi ya haraka haraka tu ambayo unaweza kuokoa elfu moja na zaidi kwenye kila siku ya maisha yako. Lakini ukiyakagua maisha yako vizuri, utaona maeneo mengi zaidi unayopoteza fedha ndogo ndogo bila ya kujua.

Rafiki, nipo hapa kwa ajili yako, naandaa mafunzo bora kwa ajili yako, na pia nafanya kila ninachoweza kuhakikisha hukosi mafunzo haya bora sana kwako. Nakuomba utekeleze wajibu wako ili mafunzo haya yaweze kukusaidia. Kama unashindwa kabisa kulipa ada ya shilingi elfu 20 ili kupata mafunzo ya TABIA ZA KITAJIRI, niandikie kwenye email maarifa@kisimachamaarifa.co.tz na nitaona njia bora ya kukusaidia ili upate mafunzo haya na uweze kuondokana na changamoto za kifedha kwenye maisha yako.

Nikukaribishe sana kwenye SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI, ambapo tutakwenda kujifunza msingi mpya wa kuyaendesha maisha yetu kwa mafanikio makubwa sana.

Kwa muhtasari; SEMINA; TABIA ZA KITAJIRI.

Semina itatupa maarifa ya kujijengea tabia kumi za kuishi kila siku ambazo zitatuwezesha kufika kwenye utajiri mkubwa.

Semina itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki ukiwa popote.

Semina itaanza tarehe 03/01/2019 mpaka tarehe 13/01/2019.

Kupata nafasi ya kushiriki semina unalipa ada ya KISIMA CHA MAARIFA (tsh 100,000/=) au kama huwezi hiyo unalipia ada ya kushiriki semina tu (tsh 20,000/=)

Unaweza kulipa ada kidogo kidogo ili mpaka kufika tarehe ya mwisho uwe umekamilisha.

Namba za kufanya malipo ni 0755 953 887 au 0717 396 253.

Mwisho wa kulipia ni tarehe 02/01/2019 ila nafasi zikijaa kabla hutapata tena nafasi.

Unaweza kumlipia mtu wa karibu kwako akajifunza.

Kujiunga na kundi la semina hii tumia kiungo hiki; https://chat.whatsapp.com/JvJBnoKixGrJZpZdw3shRv  (kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA usijiunge na kundi hili).

Karibu sana tupate maarifa sahihi ya kutujenge tabia zitakazotufikisha kwenye utajiri mkubwa.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge