“People seek retreats for themselves in the country, by the sea, or in the mountains. You are very much in the habit of yearning for those same things. But this is entirely the trait of a base person, when you can, at any moment, find such a retreat in yourself. For nowhere can you find a more peaceful and less busy retreat than in your own soul—especially if on close inspection it is filled with ease, which I say is nothing more than being well-ordered. Treat yourself often to this retreat and be renewed.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 4.3.1

Ni siku nyingine mpya na bora sana kwetu rafiki,
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka kuhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari PUMZIKO BORA LIPO NDANI YAKO…
Watu wamekuwa wanatumia muda mwingi kutafuta eneo la kupumzika kuliko muda ambao wanapumzika.
Wanapanga kwenda eneo la mbali ambapo kutakuwa na utulivu na wanaamini watapumzika vizuri, lakini hawapati pumziko zuri kokote wanakoenda.
Tena wakati mwingine kitendo cha kwenda mbali kinakuwa kazi zaidi kwao kuliko kupumzika.

Rafiki, pumziko bora kabisa kwako lipo ndani yako, linaanza na wewe kwa kutuliza akili yako popote pale ulipo.
Unaweza kutuliza fikra zako na kuzima mawazo ya nje popote pale ulipo na ukapata utulivu na pumziko bora kabisa.

Na kama huwezi kutulia pale ulipo sasa, kama huwezi kutuliza akili yako na kudhibiti fikra zako kwa pale ulipo sasa, hakuna popote utakapoenda na ukaweza kupata pumziko bora.

Pumziko bora ni matokeo ya udhibiti wa fikra zako ulionao na siyo sehemu ambayo upo. Hivyo anzia hapo ulipo sasa, kwa kudhibiti fikra zako ili kuweza kupata pumziko bora.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa na pumziko bora kwa kujipa muda wa kutuliza akili yako na kudhibiti fikra zako.
#UnapoendaNdipoUlipo, #DhibitiFikraZako, #TawalaHisiaZako

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha