Kama umewahi kukwama kwenye jambo lolote na kujiambia huna cha kufanya, umekuwa unajidanganya.

Kuna mambo mengi sana ya kufanya popote unapokuwa, lakini kwanza lazima uanze kuangalia kipi cha kufanya na utaviona vingi.

Kama huoni kitu cha kufanya, maana yake umekataa kuangalia ni kipi cha kufanya kwa pale ulipo.

Lakini ukianza kuangalia kipi cha kufanya, ukianza kujiuliza ufanye nini, utaona vitu vingi vya kufanya.

Mtu pekee ambaye hana cha kufanya ni yule ambaye ameshakufa. Lakini kama upo hai, una mengi sana ya kufanya.

Haijalishi umekwama wapi, kuna mengi unaweza kufanya ya kukutoa hapo ulipo sasa.

Kuna mengi unaweza kuifunza na kuanza upya.

Kuna watu unaweza kuongea na wakakupa mawazo ya tofauti na uliyonayo.

Na pia yapo mengi ya kujifunza kupitia safari ya maisha yako mwenyewe, na hatua bora zaidi za kuchukua kuliko ulivyokuwa huko nyuma.

Usikubali kuwa kwenye hali ambayo unajiambia huna cha kufanya, badala yake kwenye kila hali angalia kipi unaweza kufanya na kisha fanya hicho.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha