“What’s the point of having countless books and libraries, whose titles could hardly be read through in a lifetime. The learner is not taught, but burdened by the sheer volume, and it’s better to plant the seeds of a few authors than to be scattered about by many.”
—SENECA, ON TRANQUILITY OF MIND, 9.4

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UBORA NA WINGI…
Huwa tunapenda kupima maendeleo yetu kwa wingi wa tulivyonavyo au tulivyofanya.
Lakini mara nyingi wingi haufanyi maisha yetu kuwa bora.
Kufanya vitu vingi au kuwa na vitu vingi ambavyo ni vya kawaida haileti mchango wowote kwenye maisha yake.

Njia sahihi ya kupima maendeleo yako ni ubora wa vitu unavyofanya au ulivyonavyo.
Kufanya au kuwa na vitu vichache ambavyo ni borw zaidi kunayafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Unapokazana na vilivyo bora, unapiga hatua zaidi kwenye maisha.

Badala ya kutaka kusoms kila kitabu kwa haraka ili tu useme umesoma vitabu vingi, ni bora kusoma vitabu vichache vilivyo bora zaidi, ukavisoma kwa undani na kuviweka kwenye maisha yako.

Badala ya kukazana kufanya kila kitu kwenye siku yako, ni vyema kichagua machache ambayo ni muhumu zaidi na kuyafanya kwa ubora wa hali ya juu na yatakuwezesha kupiga hatua.

Badala ya kutaka kila mtu awe mteja wa biashara yako, ni vyema kuchagua wachache ambao watakuwa wateja bora kabisa, wanaoelewa na kujali thamani unayotoa na ukaweza kuwahudumia vizuri zaidi.

Kwenye kila eneo la maisha yetu, ubora unazidi wingi, hivyo achana na mbio za dunia za kukimbilia wingi, wewe kimbilia ubora.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukazana na ubora na kuachana na wingi.
#KazanaNaUbora, #AchanaNaWingi, #UboraUnazidiWingi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha