“The beautiful and good person neither fights with anyone nor, as much as they are able, permits others to fight . . . this is the meaning of getting an education—learning what is your own affair and what is not. If a person carries themselves so, where is there any room for fighting?”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 4.5.1; 7b–8a

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ambayo tumeiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KUELIMIKA KWELI NI KUEPUKA MABISHANO YA KUSHINDANA…
Wapo watu ambao wanapenda kubishana na kushinda kila aina ya ubishani, haijalishi ni mdogo kiasi gani.
Hawa ni watu ambao wanapoteza muda wao na nguvu zao kwa mambo mengi yasiyo muhimu.
Na pia ni koashiria kwamba mtu hajaelimika kweli.

Kwa sababu kuelimika kweli ni kuepuka mabishano ya kushindana,
Kuelimika kweli ni kujua yale muhimu kwako, na kuwa tayari kujifunza yale usiyojua.
Kuelimika kweli siyo kulazimisha kila mtu akubaliane na wewe, bali kuwapa watu uhuru wa kukaa upande wanaotaka wenyewe.
Kuelimika kweli ni kuwa na udadisi wa kutaka kujua kwa nini watu wamechagua upande waliopo na kuachana na ubishani usio na maana.

Kuna mambo mengi ambayo watu wanabishana kushinda, lakini hata baada ya kushinda hakuna kinachobadilika kwenye maisha yako.
Kuwa mtu uliyeelimika kweli, achana kabisa na mabishano ya kushindana.
Mara zote kazana kuujua ukweli, kama wanachosimamia wengine ndiyo ukweli basi upokee. Na kama siyo ukweli basi waache waendelee kusimamia hicho na wewe simamia ukweli.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuachana na mabishano ya kushindana.
#KubishanaNiKupotezaMuda #UtafuteUkweli #SimamiaKilichoSahihi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1