Rafiki yangu mpendwa,

Kwa zama tunazoishi sasa, kuingia kwenye biashara imekuwa ni kitu rahisi sana.

Watu wanaweza kuingia kwenye biashara bila ya mtaji au kwa mtaji kidogo sana. Na pia watu wanaweza kuingia kwenye biashara bila ya kuwa na eneo la biashara.

Mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii imerahisisha sana ufanyaji wa biashara.

Sasa kwa kuwa ni rahisi kuingia kwenye biashara, ushindani wa kibiashara umekuwa mkubwa sana. Na hili limepelekea biashara nyingi kushindwa kukua na hata kufa kabisa.

small-biz-growth-pic

Leo nakwenda kukushirikisha sababu tano kubwa zinazozuia biashara nyingi kukua na jinsi unavyoweza kuondoka kwenye mkwamo wa kibiashara na kupiga hatua zaidi.

Sababu 5 zinazozuia biashara nyingi kukua.

Moja; mmiliki wa biashara.

Mmiliki wa biashara ni kikwazo cha kwanza kabisa kwenye ukuaji wa biashara. Pale ambapo biashara inamtegemea mmiliki wa biashara hiyo kwenye kila kitu haiwezi kukua. Kama mwanzilishi wa biashara ndiye anayetegemewa kufanya kila kitu kwenye biashara, biashara haiwezi kukua.

Ili biashara kukua lazima mmiliki aweze kujitofautisha na kujitenganisha na biashara hiyo. Ajenge biashara ambayo inaweza kujiendesha yenyewe bila ya uwepo wake.

Mbili; kukosa wateja wapya.

Biashara inakua kwa kutengeneza wateja wapya kila wakati. Biashara nyingi zimekuwa hazina mfumo mzuri wa kutengeneza wateja wapya kila wakati. Hivyo wanaendelea kuwa na wateja wale wale na hilo linakuwa kikwazo kikubwa kwenye ukuaji.

Ili biashara ikue lazima iwe inatengeneza wateja wapya kila wakati. Wateja wapya ndiyo wanaoleta ukuaji wa biashara.

Tatu; kukosa wafanyakazi bora.

Wafanyakazi wa biashara ndiyo wanaoweza kuikuza au kuiangusha. Biashara nyingi hazina wafanyakazi sahihi na hilo limekuwa linazizuia biashara hizo kukua.

Wafanyabiashara wengi hawana mfumo mzuri wa kuajiri watu sahihi kwenye biashara zao na hilo limekuwa linawagharimu kwenye ukuaji. Ili biashara ikue, inahitaji kuwa na wafanyakazi bora ambao wanaweza kutekeleza majukumu yao vizuri.

Nne; mzunguko hasi wa fedha.

Fedha ndiyo damu ya biashara, mzunguko wa fedha ukiwa vizuri biashara inakua, ukiwa vibaya biashara inakufa.

Biashara nyingi zinazokufa zina mzunguko hasi wa fedha, ikiwa na maana kwamba matumizi ya biashara ni makubwa kuliko mapato.

Ili biashara ikue, inahitaji kuwa na mfumo bora wa kudhibiti mzunguko wa fedha ili uwe chanya. Mapato yawe makubwa kuliko matumizi.

Tano; mauzo yasiyotosheleza.

Mauzo ndiyo injini au moyo wa biashara. Mauzo ndiyo yanayosukuma mzunguko wa fedha kwenye biashara. Bila ya mauzo hakuna biashara.

Biashara nyingi zimekuwa hazina mauzo ya kutosheleza kuzalisha mapato yanayoiwezesha biashara hiyo kujiendesha kwa faida.

Biashara hizo hazina mfumo bora wa masoko ambao unawezesha mauzo kuwa mazuri na yanayoiwezesha biashara kujiendesha yenyewe.

Rafiki, hizi ndizo sababu tano kubwa zinazozuia biashara nyingi kukua, ukizikabili sababu hizi tano, biashara yako itaweza kukua sana.

Swali unalojiuliza ni je unawezaje kukabiliana na sababu hizo tano na kuzishinda?

Na jibu ni moja, unahitaji kuwa na mfumo sahihi wa kuendesha biashara hiyo.

JINSI YA KUONDOKA KWENYE MKWAMO WA KIBIASHARA.

Rafiki, kama umekuwa kwenye biashara kwa muda mrefu lakini haikui, basi umekwama. Na hata kama bado hujaingia kwenye biashara, unapaswa kujua mkwamo wa kibiashara ni moja ya sababu zinazowazuia wengi kukua.

Ipo njia moja pekee ya kuondoka kwenye mkwamo wa kibiashara. Njia hiyo ni KUTENGENEZA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YAKO.

Unapotengeneza mfumo, kila sababu tuliyojifunza hapo juu inatengenezewa njia bora ya kuitekeleza na hivyo inaacha kuwa kikwazo kwenye ukuaji wa biashara yako.

Kutengeneza mfumo ni kitu ambacho kitakupa wewe uhuru wa biashara yako, kwa biashara kuweza kujiendesha yenyewe bila ya wewe kuwepo moja kwa moja.

Lakini pia mfumo utakuwezesha kuajiri watu sahihi wa biashara yako, kutengeneza wateja wapya kila siku, kudhibiti mzunguko wa fedha na kuongeza mauzo zaidi.

Kama unataka mafanikio makubwa kwenye biashara, jibu lipo kwenye mfumo.

Swali ni je unawezaje kutengeneza mfumo wa kuendesha biashara yako?

Na hapo ndipo nimekuandalia semina maalumu ya kukusaidia kutengeneza mfumo wa biashara yako.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Rafiki, baada ya kuona changamoto kubwa ambazo wafanyabiashara wengi wanapitia, hasa ya kukosa uhuru licha ya kuwa kwenye biashara. Na baada ya kujifunza na kutafiti kwa kina, nimekuandalia semina nzuri ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki semina hii ukiwa popote duniani, na huhitaji kusafiri au kuacha shughuli zako za kila siku, ni kutenga tu muda ndani ya siku yako wa kufuatilia masomo ya semina.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi, ambapo kila siku utapata somo la jinsi ya kutengeneza mfumo kwenye biashara yako. Masomo haya yatakuwa na mifano halisi ya hatua unazopaswa kuchukua ili biashara yako ijiendeshe kwa mfumo. Pia utapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi zaidi kwenye maeneo ambayo hayajaeleweka.

Semina hii itaanza rasmi tarehe 04/07/2019 mpaka tarehe 14/07/2019, kila siku asubuhi utapata somo la semina na utaweza kuuliza maswali kuhusiana na somo hilo. Masomo yote yatatumwa kwenye kundi la wasap na hivyo utaweza kuyafuatilia kwa urahisi.

Japokuwa semina hii inafanyika kwa njia ya mtandao, utajifunza kwa kina sana na kuondoka na mengi ya kwenda kufanyia kazi kuliko unavyoweza kujifunza kwenye semina ya kuhudhuria ana kwa ana. Kwa sababu semina hii ya mtandaoni inakwenda kwa kina sana kitu ambacho siyo rahisi kukifanya kwenye semina ya siku moja ya ana kwa ana.

JINSI YA KUSHIRIKI SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA.

Rafiki, ili uweze kushiriki semina hii nzuri sana itakayokupa uhuru kamili wa maisha yako, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii itaendeshwa moja kwa moja kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya programu za mafunzo na ukocha ninayoendesha, ambapo watu wanajifunza na kuhamasika kila siku, kisha kuchukua hatua na maisha yao kuwa bora sana.

Kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ada yako iko hai basi tayari umeshajihakikishia kushiriki semina hii. Wewe jiandae tu, kaa mkao wa kujifunza na utaondoka na nondo za kwenda kuiendesha biashara yako vizuri.

Kama ni mwanachama lakini ada yako inaisha karibuni, lipa ada yako mapema ili usikose nafasi ya kushiriki semina hii. Hakikisha hutoki ndani ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kunufaika zaidi na mafunzo haya na mengine mengi.

Kama wewe siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina hii ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO, unapaswa kujiunga na kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Hapa unalipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima tangu tarehe uliyolipia. Utapata mafunzo ya semina mbili zinazofanyika mtandaoni kwa mwaka, na pia utapata nafasi ya kuwa karibu na mimi kocha wako, tukijifunza kwa kina. Pia tunakwenda kuwa ka Klabu za KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinakupa jumuiya ya watu ulionao karibu ambao wanapiga hatua kufanikiwa zaidi.

JINSI YA KULIPA ADA.

Ili kulipa ada ya kushiriki semina hii, tuma kwenye namba zifuatazo;

TIGO PESA / AIRTEL MONEY – 0717 396 253 (Jina AMANI MAKIRITA)

M-PESA – 0755 953 887 (Jina AMANI MAKIRITA)

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa wasap  kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA.

MWISHO WA KULIPIA ILI KUSHIRIKI SEMINA.

Rafiki, mwisho wa kulipia ada yako ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kupata mafunzo ya semina hii ni tarehe 01/07/2019.

Ili ujihakikishie kushiriki semina hii na kuweza kuikuza biashara yako, lipa ada yako mapema kabla ya tarehe hiyo ya mwisho.

Ninaamini unapenda sana kupiga hatua na kufanikiwa kwenye biashara yako,

Ninaamini hilo linawezekana kabisa, kwa sababu nimeona wengi wakianzia chini na kupiga hatua zaidi.

Na nina imani kubwa kwenye mafunzo niliyokuandalia, yanakwenda kukupa uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako, hata kama biashara yako ni ndogo sana.

Karibu sana ushiriki semina hii ya MFUMO WA BIASHARA na utaweza kupiga hatua zaidi. Kumbuka kulipa ada yako kwa wakati, kabla ya tarehe 01/07/2019 ili uweze kunufaika na mafunzo haya yatakayoiwezesha biashara yako kukua zaidi.

Nakusubiri kwa shauku kubwa kwenye semina hii ya MFUMO WA BIASHARA, kwa sababu najua utaondoka na mengi ya kuiwezesha biashara yako kukua zaidi. Usipange kukosa semina hii.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge