“At this moment you aren’t on a journey, but wandering about, being driven from place to place, even though what you seek—to live well—is found in all places. Is there any place more full of confusion than the Forum? Yet even there you can live at peace, if needed.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 28.5b–6a

Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MAISHA MAZURI YAPO KILA MAHALI…
Mara nyingi tumekuwa tunajiambia kwamba tutakuwa na maisha mazuri kama tutafanya kazi fulani au biashara fulani.
Au tunajiambia tutakuwa na maisha mazuri kama tukiishi eneo fulani, au tukiwa na mali fulani.
Lakini hii yote ni kujidanganya na kujichelewesha kuwa na maisha mazuri.

Maisha mazuri yapo kila mahali, yapo kwenye kila kazi na kila biashara, yapo kwenye kila eneo na yapo kwenye kila kiwango cha mali ambacho mtu anacho.
Ni wewe kuchagua kuwa na maisha mazuri na maisha yako yanabadilika kabisa.

Anzia hapo ulipo sasa, kwa kile unachofanya sasa na kwa mali ulizonazo sasa.
Chagua kuwa na maisha mazuri, na anza kuishi maisha mazuri.
Maisha mazuri ni pale ambapo upo tayari kupokea chochote kinachokuja kwako bila ya kutetereka.
Maisha mazuri ni pale ambapo unajitoa kwenye kile unachofanya, ili kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi.
Maisha mazuri ni pale unapokazana kukua zaidi wewe binafsi na kupiga hatua kwenye maisha yako.

Usisubiri chochote, anza kuwa na maisha mazuri hapo ulipo sasa, kupitia kila unachofanya sasa.
Maisha mazuri yapo kila mahali, usihangaike kuyakimbiza, bali yavutie yaje hapo ulipo.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutengeneza maisha mazuri kwa kuanzia hapo ulipo sasa.
#MaishaMazuriYanatengenezwa #UsihangaikeKukimbizaMaisha #AnziaHapoUlipoSasa

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1