Rafiki yangu mpendwa,
Unanijua leo hii kwa sababu moja tu, USOMAJI WA VITABU.
Unanufaika na kazi mbalimbali ninazozifanya kupitia uandishi na ukocha kwa sababu moja tu, USOMAJI WA VITABU.
Ni kupitia usomaji wa vitabu ndipo maisha yangu yalibadilika kabisa, kwa kuweza kuvuka moja ya vipindi vigumu kabisa kwenye maisha yangu na kuweza kusimama mpaka leo hii.
Kama isingekuwa usomaji wa vitabu, leo hii usingenijua mimi na wala usingeweza kunufaika na chochote ninachofanya sasa.
Ndiyo maana nimekuwa nasisitiza sana kila mmoja wetu ajifunze kupitia usomaji wa vitabu.
Leo tarehe 03/08/2019 ni siku ya uzinduzi wa vitabu viwili nilivyotoa, ambavyo ni ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, kitabu kinachokupa maarifa sahihi ya kifedha na kitabu, TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA ambacho ni mwongozo sahihi wa mafanikio, kitabu utakachokisoma kwa mwaka mzima.
Katika uzinduzi wa leo, moja ya vitu nitakavyokushirikisha ni jinsi ambavyo usomaji wa vitabu ulivyobadili kabisa maisha yangu na leo hii ukaweza kunijua na kunufaika na kazi mbalimbali ninazofanya.
Nichukue nafasi hii kukukaribisha sana kwenye uzinduzi wa vitabu hivi viwili muhimu.
Uzinduzi unafanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Park iliyopo Sinza dar es salaam. Uzinduzi unaanza saa nane kamili mchana mpaka saa 12 kamili jioni, karibu sana tujumuike pamoja na kuweza kujifunza kuhusu usomaji wa vitabu.
Kushiriki uzinduzi huu utalipia kiingilio cha shilingi elfu kumi (10,000/=) ambayo utailipa wakati wa kuingia ukumbini.
Pamoja na kujifunza mengi kuhusu usomaji wa vitabu, lakini pia utavipata vitabu kwa bei ya punguzo.
Pia utapata nafasi ya kuwekewa sahihi kwenye vitabu vyako na mwandishi na kupata picha ya pamoja na mwandishi wa vitabu. Sasa kama unavyojua malengo yangu makubwa mawili, kuwa BILIONEA na kuwa RAISI WA TANZANIA, moja ya vitu vya thamani sana unavyoweza kumiliki kwenye maisha yako ni kuwa na kitabu ambacho nimekiwekea sahihi na kuwa na picha ya pamoja.
Karibu sana kwenye uzinduzi huu, fika mapema ili uweze kujifunza na kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
Kwa wale ambao hawatashiriki uzinduzi moja kwa moja, karibu ujipatie vitabu kwa bei ya punguzo hapo hapo kwenye ukumbi wa uzinduzi.
Lakini pia utapata nafasi ya kuwekewa sahihi kwenye vitabu ulivyonunua bure kabisa na kupata picha ya pamoja na mwandishi. Zoezi la kuweka sahihi vitabu na kupiga picha litafanyika kuanzia saa nane kamili mchana mpaka saa tisa kamili. Fika muda huo na utapata vitabu, sahihi na picha bure kabisa.
Jinsi ya kufika kwenye ukumbi ambao uzinduzi utafanyika; panda magari au pita barabara ya shekilango na shuka kituo kinachoitwa Sinza kumekucha. Hapo utaliona kanisa la KKKT, lenye msalaba mwekundu juu. Fuata njia hiyo ambapo kanisa lipo na mbele kidogo utaiona GOLDEN PARK HOTEL, ingia hapo na uliza ukumbi wa mikutano na utaelekezwa.
Karibu sana rafiki yangu, leo ni siku ambayo hupaswi kuikosa, kwani ni siku ya kihistoria, siku utakayopata vitabu, mafunzo mazuri kuhusu vitabu, sahihi kwenye vitabu vyako pamoja na picha ya pamoja na mwandishi wa vitabu.
Kwa maelezo zaidi jinsi ya kufika kwenye uzinduzi au kupata vitabu piga simu namba 0678 977 007 au 0752 977 170.
Karibu sana rafiki, usikubali nafasi hii bora sana ya leo ikupite, karibu kwenye uzinduzi na utaondoka na maarifa na hamasa sahihi ya kwenda kuyabadili kabisa maisha yako kupitia usomaji wa vitabu.
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.