Rafiki yangu mpendwa,

Kupitia vitabu viwili vipya nilivyotoa, ELIMU YA MSINGIYA FEDHA na TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA nilitoa zawadi ya kupata vitabu hivi kwa bei ya punguzo.

Kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA ambacho kinakupa maarifa yote muhimu ya kifedha, ambayo hujawahi kufundishwa popote kilipatikana kwa bei ya zawadi ambayo ilikuwa tsh elfu 15 badala ya elfu 20.

Kitabu TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA, ambacho ni mwongozo mkuu wa mafanikio wa kusoma kwa mwaka mzima, chenye uchambuzi wa vitabu 50 vya mafanikio, kilipatikana kwa bei ya zawadi ambayo ilikuwa tsh elfu 40 badala ya elfu 50.

Zawadi hii ya vitabu ilifika mwisho wake tarehe 31/07/2019. Licha ya zawadi hiyo kufika mwisho bado watu wengi wamekuwa wanahitaji kuendelea kupata zawadi hiyo. Lakini imeshindikana kwa sababu muda umeshapita.

Leo nina habari njema kabisa kwa wale wote ambao wameikosa zawadi ya vitabu kwa bei ya punguzo. Kuna siku moja pekee ambapo unaweza kujipatia tena vitabu hivi kwa bei ya zawadi.

Siku hiyo ni siku ya uzinduzi wa vitabu hivyo, ambayo itakuwa ni jumamosi ya tarehe 03/08/2019. Uzinduzi huu utafanyika kwenye hoteli ya Golden Park iliyopo Sinza dar es salaam. Uzinduzi utaanza saa nane kamili mchana mpaka saa 12 jioni. Kwenye uzinduzi huu utajifunza mambo mengi muhimu kuhusu usomaji wa vitabu, pamoja na njia bora za kusoma vitabu.

TANGAZO LA UZINDUZI VITABU (2)

Siku hiyo ya uzinduzi wa vitabu, utavipata kwa bei ya punguzo badala ya bei kamili. Hivyo unaweza kufika na kujipatia vitabu vyako kwa bei ya punguzo.

Hata kama hautashiriki semina ya uzinduzi, unaweza kufika na kujipatia vitabu peke yake. Na kama uko mkoani na ungependa kupata zawadi hii kwa siku hiyo ya semina, utatuma malipo ya vitabu na majina ya vitabu ulivyolipia, majina yako na ulipo ili uweze kupata zawadi hiyo ya vitabu. Malipo yatumwe kwa namba 0717396253 au 0755953887, majina ya namba hizo ni Amani Makirita.

Rafiki, hii ni nafasi ya mwisho kabisa kwako kupata zawadi hii ya vitabu, itumie sasa ili usiikose tena.

Kwa wale watakaoshiriki semina ya uzinduzi, itaanza saa nane kamili mchana mpaka saa 12 jioni. Jinsi ya kufika eneo la uzinduzi, ni kituo cha sinza kumekucha, karibu na kanisa la KKKT Sinza. Ukifika hapo ulizia hotel ya Golden Park na utaweza kufika hotelini na kuelekezwa ukumbini.

Kama hukuweka nafasi ya kushiriki uzinduzi lakini unahitaji kushiriki, tuwasiliane sasa kwa namba 0717396253, kuna nafasi chache zinapatikana.

Karibuni sana wote tujumuike pamoja kwenye uzinduzi wetu wa vitabu pamoja na kujipatia vitabu kwa bei ya punguzo. Imebaki siku hiyo moja tu ya uzinduzi, kila mmoja wetu aitumie vizuri ili asikose zawadi na nafasi hiyo ya kujifunza.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.