“Won’t you be walking in your predecessors’ footsteps? I surely will use the older path, but if I find a shorter and smoother way, I’ll blaze a trail there. The ones who pioneered these paths aren’t our masters, but our guides. Truth stands open to everyone, it hasn’t been monopolized.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 33.11
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ambayo tumeiona leo.
Hii ni nafasi ya kipekee na bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Tusimamie hayo matatu na siku hii itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari IHESHIMU JANA NA KUWA TAYARI KWA KESHO…
Kuna mambo mengi sana ambayo umejifunza kwa wale waliokutangulia,
Lakini hiyo haimaanishi kwamba kila ulichojifunza ndiyo sahihi.
Unayo nafasi ya kuboresha zaidi kile ambacho umejifunza.
Hivyo badala ya kuwa mtumwa wa yale uloyojifunza siku za nyuma, kuwa huru kwa kuwa tayari kujifunza kwa wengine zaidi kesho.
Using’ang’ane na kile ulichojifunza huko nyuma kama kuna mapya na mazuri zaidi uliyojifunza leo.
Heshimu yale uliyojifunza siku zilizopita, lakini kuwa tayari kuyaboresha zaidi kadiri unavyopata taarifa na maarifa mapya.
Na ndiyo maana kujifunza hakuna mwisho, kwa sababu ukilinganisha yale unayojiambia unajua na yake usiyojua, ni kama tone la maji kwenye bahari kubww.
Kama amnavyo Seneca anatuambia, jukumu letu ni kuutafuta ukweli, kwa sababu ukweli haujahodhiwa na mtu yeyote yule, ukweli uko wazi kwa kila mmoja wetu, ni wewe kuukubali na kuutumia kwenye maisha yako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuendelea kujifunza na kuutafuta ukweli ili kuyaboresha maisha yetu zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1