“Whenever you take offense at someone’s wrongdoing, immediately turn to your own similar failings, such as seeing money as good, or pleasure, or a little fame—whatever form it takes. By thinking on this, you’ll quickly forget your anger, considering also what compels them—for what else could they do? Or, if you are able, remove their compulsion.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 10.30
Ni siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi hii nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA ,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari FIKIRIA MAKOSA YAKO PIA…
Kuna wakati ambao watu wengine huwa wanafanya makosa ambayo yanatuudhi, kutukasirisha, kutukwamisha na hata kutukatisha tamaa.
Katika nyakati kama hizo ni rahisi sana kukasirika na kuwachukia watu hao na kuwaona kama ni kikwazo kwetu.
Lakini hilo halitusaidii sisi na wala haliwasaidii wao.
Mara nyingi watu hukosea siyo kwa makusudi, bali kwa kutokujua.
Na kudhibitisha, jikumbushe makosa ambayo umewahi kufanya huko nyuma.
Mara zote hukukaa chini na kujiambia leo nataka nimfanyie mtu makosa,
Badala yake ulijikuta umeshafanya makosa, labda kwa kusahau, kwa kupitiwa, kwa kutokuelewa vizuri au hata kuwa na njia njema ambayo baadaye iligeuka na kutokuwa nia njema tena.
Kwa kufikiria hivi, hatua sahihi kuchukua kwa wale wanaotukosea ni kuwasamehe, kutokuwachukia au kubebw vinyongo juu yao.
Badala yake kujua wamejaribu kadiri ya uwezo wao ila wamekwama hapo.
Tujue na sisi pia tuna nafasi kubwa ya kuendelea kufanya makosa mbalimbali, lakini tujitahidi kuwa bora zaidi kila siku.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya leo kujikumbusha makosa yetu ili kupata nafasi ya kiwasamehe wale ambao wanatukosea pia.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1