“The art of living is more like wrestling than dancing, because an artful life requires being prepared to meet and withstand sudden and unexpected attacks.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 7.61
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii mpya tuliyoiona leo,
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAISHA SIYO NGOMA, NI MIELEKA…
Kucheza ngoma ni rahisi, kazi kwako ni kwenda na mdundo na stepu ambazo wanapiga wengine.
Hakuna anayeweza kukushambulia ukiwa unacheza ngoma, ni kitendo cha kistaarabu na kila mtu anafurahia.
Hivi ndivyo tunavyopenda maisha yetu yangekwenda, lakini huo siyo uhalisia.
Maisha siyo sawa na uchezaji wa ngoma, bali ni sawa na uchezaji wa mieleka.
Kwenye mieleka hakuna chochote kinachotabirika. Mshindani wako anaweza kukuvizia na kukushambulia ukiwa hujajiandaa vyema na hivyo kukuangusha vibaya.
Angalia ni nyakati gani maisha yamekuwa yanakupiga mweleka, ni nyakati ambazo hukuwa na maandalizi kabisa, nyakati ambazo hukujua kilichotokea kingeweza kutokea, na kinatokoea na kukuacha ukiwa na mshangazo.
Maisha ni mieleka, wakati wowote unapaswa kuwa na maandalizi ya kukabiliana na mashambulizi ambayo huyategemei.
Na falsafa ni moja ya njia zinazoweza kukuimarisha na ukaweza kukabiliana na chochote kinachotokea kwenye maisha yako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujiandaa vyema kwa mashambulizi ambayo mtu hutegemei kukutana nayo, maana maisha huwa yana tabia ya kutushangaza sana.
#MaishaNiMieleka #MaraZoteKuwaNaMaandalizi #FalsafaNiKiungoChaUimara
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1