“For even peace itself will supply more reason for worry. Not even safe circumstances will bring you confidence once your mind has been shocked—once it gets in the habit of blind panic, it can’t provide for its own safety. For it doesn’t really avoid danger, it just runs away. Yet we are exposed to greater danger with our backs turned.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 104.10b

Ni siku mpya,
Siku bora na ya kipeke sana kwetu.
Tumeiona nafasi hii nyingine bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MAFANIKIO HAYABADILISHI, YANAZIDISHA…
Kumekuwa na malalamiko kwamba watu wakishafanikiwa basi wanabadilika.
Kwamba kabla hawajafanikiwa walikuwa na tabia fulani, lakini baada ya kufanikiwa tabia zao zinabadilika kabisa.
Hili siyo sahihi, mafanikio huwa hayawabadilishi watu, bali huwa yanakuza kile kilicho ndani yao.
Kabla ya mtu kufanikiwa, kuna tabia tunakuwa hatuzioni kwa nje kwa sababu hana nafasi kubwa ya kuzionesha.
Lakini mtu anapofanikiwa, anakuwa na nafasi kubwa ya kuonesha tabia zake hizo na hivyo tunaziona kwa wazi zaidi.

Upande wa pili wa hili ni usitegemee mafanikio zaidi yataondoa kile kinachokusumbua ndani yako.
Mfano kama una hofu ya kupoteza, kadiri unavyofanikiwa, ndivyo hofu hiyo inakuwa kubwa zaidi.
Kama una milioni moja na unahofia kuipoteza, ukiwa na milioni mia moja hofu hiyo haiondoki, bali inakuwa kubwa zaidi.

Hivyo tunapokazana kufanikiwa zaidi, tujue wazi ya kwamba mafanikio hayo hayatabadili kile kilicho ndani yetu, bali yatakikuza zaidi.
Hivyo kama kuna vitu tunataka kubadili kwenye maisha yetu, basi tunapaswa kuhangaika navyo moja kwa moja na siyo kutegemea mafanikio zaidi yatabadili vitu hivyo.
Nenda moja kwa moja kwenye tabia unazotaka kubadili na zifanyie kazi, usitegemee mafanikio yalete mabadiliko yoyote.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanyia kazi tabia zetu ili kuleta mabadiliko bora na siyo kutegemea mafanikio yalete mabadiliko hayo.
#MafanikioHayakubadilishi #MabadilikoYanaanziaNdani #KablaHukafanikiwaBadilika

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1