Kwenye maisha yako, jihusishe na watu ambao tayari wana furaha kwa hali yoyote wanayopitia kwa wakati walionao. Na siyo watu wasiokuwa na furaha, kwa kuamini kwamba utaweza kuwapa furaha.
Huwezi kumbadili mtu asiye na furaha akawa na furaha, kwa sababu kinachowakosesha furaha siyo kitu cha nje, bali kitu kilichopo ndani yao.
Watu wasio na furaha wamechagua kutokuwa na furaha na hakuna chochote unachoweza kufanya kikabadili hali hiyo waliyochagua.
Kuna tabia ambazo watu wanakuwa wamechagua kwenye maisha yao, ambazo zinachangia wasiwe na furaha, hakuna unachoweza kufanya ukabadili hali hiyo.
Hivyo usipoteze muda na nguvu zako kutaka kuwafanya wengine wawe na furaha, chagua kuyaishi maisha yako na kushirikiana na wale ambao tayari wana furaha.
Na kama wewe ndiye mtu usiyekuwa na furaha na unayetegemea kupata furaha kutoka kwa wengine, ni wakati sasa wa kuacha kupoteza muda kutafuta kitu ambacho hujapoteza. Badala yake kaa na angalia ndani yako, na ona ni wapi unapojikwamisha usiwe na furaha.
Kama unaona maisha yako hayafai, maisha hayako sawa kwako na dunia inakutenga, chukua nafasi na tembelea hospitali yenye wagonjwa mahututi au tembelea gereza na ongea na watu waliofungwa kwa muda mrefu, ukitoka hapo, utaona jinsi ambavyo una kila cha kushukuru na kufurahia kwa kutokuwa mgonjwa au mfungwa.
Na hata kama una ugonjwa sugu au umefungwa, fikiria wale ambao wameshafariki, tena kwenye mazingira magumu, lakini wewe bado unaivuta pumzi, ni jambo la kushukuru na kufurahia sana.
Nimalizie kwa kukuambia, watu wasiokuwa na furaha wana kisirani chao wenyewe, kaa nao mbali, maana watakuambukiza kisirani hicho.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Asante kocha Kwa ujume huu mzuri. Furaha ni uchaguzi wa mtu. Mimi nimechagua kuwa na furaha Kwa chochote ninachopitia kiwe kizuri au kibaya. Ubarikiwe Sana.
LikeLike
Hongera sana Tumaini kwa kuchagua furaha.
LikeLike
Ahsante kocha hli sitkatika furaha tu wapo watu waliojaribu kufanya vitu wakakwama na wewe unapoamua kwenda kuwasikiliza watu hao lazima utakuwa kama wao hakuna la kujifunza kwa wakatisha tamaa wao walishakata tamaa huna unachoweza kukifanya kuondoa hali ya wao kukata tamaa
LikeLike
Ni kweli Hendry,
Ni kosa kubwa sana kuchukua ushauri kutoka kwa walioshindwa na kukata tamaa.
LikeLike