Na wewe pia unaweza kufanya, kama utachukua muda na kujifunza jinsi ya kufanya kitu hicho.
Najua hii inaonekana kama kauli ya kiuhamasishaji na kuna watu huwa hawapendi kauli za kuhamasisha, kwa kusema hazina uhalisia, lakini zina uhalisia sana, na nguvu ya kukusukuma kufanya na kuwa chochote unachotaka kuwa.
Tukirudi kwenye kauli hiyo ya kama wengine wanaweza kufanya na wewe unaweza pia, kila mmoja wetu ameshawahi kumwona mtoto mchanga. Kitu pekee ambacho mtoto mchanga anazaliwa akijua kukifanya ni kunyonya na kuhakikisha anapata nyonyo (kulia pale anapotaka kunyonya).
Vitu vingine vyote, mtoto huyo anajifunza kupitia mazingira, kupitia jamii, kupitia elimu na hata kupitia juhudi binafsi. Kulingana na makuzi yake, kuna vitu atavipendelea zaidi kuliko vingine, hapa ndipo wengi huita kipaji. Lakini hakuzaliwa na kipaji hicho, bali kilijengeka kulingana na mazingira aliyokulia.
Hivyo basi, unapowaona watu wengine wanafanya mambo makubwa kwenye maisha yao, jua na wewe unaweza kufanya mambo makubwa kama wao, ila utahitaji kuweka juhudi kubwa kwenye kujifunza na kuchukua hatua ili kuweza kufikia viwango hivyo ambavyo wengine wameweza kufikia.
Kitu pekee kinachoweza kukuzuia usiwe vile unavyotaka ni wewe mwenyewe, ukishaondoa kikwazo kwenye fikra zako, nguvu kubwa iliyopo ndani yako itaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
Hebu okoa muda unaotamani ungekuwa na mazingira mazuri kama ya wengine na peleka muda na nguvu hizo katika kujifunza na kuchukua hatua ili kufika popote unapotaka kufika. Kwa sababu popote unapoona wengine wamefika, na wewe unaweza kufika pia kama utaweka juhudi sahihi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kama kuna wengine wanaweza kufanya na mimi naweza kufanya bia nikapiga hatua , asante sana kocha nitajifunza kwa kila kitu ambayo ninataka kukifanya.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike