Watu wengi wanakosa uhuru kwenye maisha yao kwa sababu mtazamo walionao kwenye uhuru ni mtazamo wa tofauti.
Wengi wanachukulia uhuru ni kuwa na kila unachotaka kwa wakati unaokitaka.
Lakini hiyo siyo sahihi, uhuru hautokani na kuwa na kila unachotaka.
Uhuru unaanzia kwenye mahitaji, na kadiri unavyokuwa na mahitaji machache kwenye jambo lolote lile, ndivyo unavyozidi kuwa huru.
Tukianzia kwenye fedha, kama mahitaji yako ni machache, ndiyo unavyozidi kuwa na uhuru mkubwa. Hata kama kipato chako siyo kikubwa, kwa sababu mahitaji yako ni machache, unakuwa huru zaidi. Tofauti na yule ambaye uhuru kwake ni kupata kila anachotaka, hata awe na fedha nyingi kiasi gani, bado kuna kitu ataona anakosa.
Hata kwenye mahusiano yetu na wengine, kadiri unavyokuwa na utegemezi mdogo kwa wengine, ndivyo unavyokuwa huru kwenye mahusiano hayo. Lakini kama una utegemezi mkubwa kwa mwingine, unakosa uhuru katika mahusiano hayo. Mfano mzuri ni kwenye ajira, kama unaitegemea ajira yako kwa kila kitu kwenye maisha yako, unakosa uhuru wa kuifanya kwa namna sahihi kwako, kwa sababu unailinda isipotee. Lakini inapotokea kwamba huitegemei ajira hiyo kwa kila kitu, kwamba hata ikipotea sasa haitakusumbua kuendesha maisha yako, unakuwa huru kuifanya kwa namna bora zaidi kwako.
Hivyo rafiki, kwa kuwa mafanikio yanaanzia kwenye uhuru, na kwa kuwa uhuru unaanzia kwenye mahitaji machache ambayo mtu unakuwa nayo, utafanikiwa zaidi kwa kuwa na mahitaji machache.
Anzia kwenye kudhibiti mahitaji yako na utakuwa huru na mwenye mafanikio zaidi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ahsante kocha kufikia uhuru ninaoutaka yanibidi niwe na mahtaji ya msingi machache na kutokuwa na utegemezi
Kweli hata upate kwa kiwańgo gani mahitaji unayotaka hutaridhika kupata uhuru
Kumbe kuna mahitaji usipokuwa nayo ndivyo unakuwa na uhuru mkubwa zaidi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nashukuru kocha kwa Makala hii kwa hiyo kwenye Uhuru huu Kitu cha msingi ni kutoendeshwa na mahitaji ya ziada au tunahitaji kujidhibiti maana naona kama inaweza kumfanya mtu akaridhika zaidi na yale mahitaji muhimu tu ya maisha yaani basic need tu, ASANTR
LikeLike
Karibu Martin.
LikeLike