“Hecato says, ‘I can teach you a love potion made without any drugs, herbs, or special spell—if you would be loved, love.’”
—SENECA, MORAL LETTERS, 9.6

Kuiona siku hii nyingine mpya na nzuri sana ya leo, ni bahati ya kipekee sana kwetu.
Siyo kww nguvu wala ujanja wa yeyote, bali ni kwa rehema tu.
Tunapaswa kuitumia siku hii vyema, kwa kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KAMA UNATAKA KUPENDWA, PENDA…
Ipo dawa moja ya uhakika ya kukuhakikishia wewe kupendwa na yeyote unayetaka akupende, anza kumpenda yeye kwanza.
Unataka watu wako wa karibu wakupende na kukujali, anza kuwapenda na kuwajali wao kwanza.
Kama unataka wateja wa biashara yako wakupende na kuja kwenye biashara yako, anza kuwapenda wao kwanza.
Hata kama kuna watu wanakuchukia, wewe wapende.

Upendo ni jawabu, upendo ni tiba na upendo hauumizi.
Chuki haijawahi kuleta matokeo yoyote mazuri,
Chuki haijawahi kuimarisha mahusiano,
Chuki haijawahi kuwageuza wenye chuki.
Upendo pekee ndiyo wenye nguvu.
Nenda katumie nguvu ya upendo leo na kila siku ya maisha yako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kusimamia upendo, siku ya kusambaza upendo kwa kila anayekuzunguka. Wapende watu kweli na wapende kutoka moyoni na wao watakulipa kwa kukupenda pia.
#SambazaUpendo #UpendoNiTiba #KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1