Watu wamekuwa wanatafuta sana mbinu za mafanikio. Wanaamini mbinu hizo zitawawezesha kupiga hatua kubwa.
Ni kweli mbinu zinaweza kuleta matokeo ya tofauti, lakini mbinu ni kitu cha muda mfupi. Mbinu inaweza kutumiwa na yeyote na kama huna njia nyingine, washindani wako wanaweza kuitumia kukusumbua.
Unachohitaji ili kufanikiwa siyo mbinu, bali mkakati. Mkakati ndiyo unaobeba mbinu ndani yake, na mkakati unakuwa na mbinu nyingi ambazo zinapotumika kwa pamoja, zinaleta matokeo ya tofauti kabisa.
Hivyo, mbinu ni kile unachofanya na mkakati ni mpango wa jinsi unavyofanya kitu hicho.
Badala ya kukimbizana na mbinu mpya za mafanikio kila siku, ambazo zinabadilika, kwanza jiwekee mkakati wako wa mafanikio. Ukishakuwa na mkakati, ni rahisi kuona mbinu ipi ufanyie kazi na ipi usifanyie kazi.
Kama huna mkakati, kila mbinu itakuwa sahihi kwako na mwishowe hutajua ni nini unafanya au wapi unakwenda.
Anza na mkakati kisha weka mbinu chini ya mkakati ulionao, kwa njia hii, huwezi kupotea.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Asante sana kocha ,nimejifunza haya naanza kuyafanyia kazi asante sana
LikeLike
Karibu James.
LikeLike