Rafiki yangu mpendwa,

Siku za karibuni nimekupa taarifa ya kutoka kwa toleo la pili la kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, kitabu ambacho kinakupa maarifa na mwongozo sahihi wa kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa umeajiriwa.

Toleo la kwanza la kitabu hiki lilitoka mwaka 2016 na tangu hapo limekuwa msaada mkubwa kwa wengi. Wale ambao walikuwa wanaona ajira zimekuwa kikwazo kwao, baada ya kusoma kitabu na kuchukua hatua, fursa nyingi zimefunguka kwao.

Na hapa ndipo niliposukumwa kutoa toleo la pili la kitabu hicho mwaka huu 2019. Toleo hilo lina mafunzo yote ya toleo la kwanza, lakini pia kuna mafunzo ya ziada, pamoja na shuhuda za wale waliosoma toleo la kwanza na kuchukua hatua.

makirita cover 3-01

Kumekuwa na watu ambao wanaomba kupata matoleo yote mawili ya kitabu, yaani toleo la kwanza na toleo la pili.

Rafiki, huhitaji kupata toleo la kwanza na la pili, unahitaji kupata toleo la pili pekee. Kwa sababu toleo la pili lina mafunzo yote ya toleo la kwanza, na mengine ya ziada.

Mafunzo ya ziada yaliyopo kwenye toleo la pili ni shuhuda kumi za wale walioanza biashara wakiwa kwenye ajira, michanganuo ya biashara 12 unazoweza kuanza kufanya ukiwa kwenye ajira, mfumo bora wa kuendesha biashara yako ukiwa kwenye ajira na njia bora ya kupata wazo la biashara, mtaji wa kuanza na muda wa kuendesha biashara yako.

Toleo la pili la kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA ni kubwa zaidi kuliko toleo la kwanza. Hivyo chukua hatua ya kupata toleo la pili na utakuwa umepata mafunzo yote ya toleo  la kwanza.

Bei ya kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA toleo la pili ni tsh elfu 20, lakini kwa sasa kuna zawadi kwako rafiki yangu, unaweza kukipata kwa tsh elfu 15 kama utakinunua kabla ya tarehe 31/10/2019.

Chukua hatua ya kukipata kitabu chako leo, tuma ujumbe au piga simu kwenda namba 0678 977 007 na utaletewa kitabu ulipo (kama upo dar) au utatumiwa kama upo mkoani.

Usichelewe kupata zawadi yako rafiki yangu, chukua hatua leo.

Maswali mengine ambayo yamekuwa yanaulizwa kuhusu kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA toleo la pili;

Swali; je naweza kupata nakala tete (softcopy) ya kitabu hiki?

Jibu; hapana, toleo la pili lipo kwa nakala ngumu (hardcopy) pekee. Nakala tete unaweza kuipata ya toleo la kwanza, ambayo ni tsh elfu 10 na unatumiwa kwa email.

Swali; vipi kama sijaajiriwa, kitabu hicho kinaweza kunisaidia?

Jibu; ndiyo, kitakusaidia sana, muhimu ni uwe tayari kuingia kwenye biashara, kitabu kina mafunzo na miongozo mingi ya kukusaidia kufanikiwa kwenye biashara.

Swali; sijui wapi pa kuanzia, je kitabu kitaweza kunisaidia?

Jibu; ndiyo, kitabu kinaweza kukusaidia kama tu utakuwa na nia ya kutoka pale ulipo sasa na kupiga hatua. Huhitaji kujua wapi pa kuanzia, kitabu kitakusaidia kujua wapi pa kuanzia na nini uanze nacho. Muhimu ni uwe na nia ya kweli.

Pata kitabu chako leo rafiki, uweze kutoka pale ulipokwama sasa na kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako kupitia biashara. Kwa sababu biashara ndiyo kitu pekee kinachoweza kukupa uhuru wa muda, fedha na maisha kwa ujumla.

Jipatie zawadi yako ya kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA toleo la pili kwa kutuma ujumbe au kupiga simu kwenda namba 0678 977 007.

Karibu sana.