“Dig deep within yourself, for there is a fountain of goodness ever ready to flow if you will keep digging.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 7.59

Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi nyingine bora kwetu kwenda kuchukua hatua kubwa ili kuweza kupata matokeo ya tofauti kwenye maisha yetu.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari CHEMCHEM YA WEMA…
Chemchem ya wema ipo ndani yako,
Kazi yako kubwa ni kuchimba ndani yako mpaka ukitane na chemchem hiyo isiyokauka.
Usitegemee wema utoke nje na kuja kwako,
Bali wema unaanzia ndani yako.
Usitegemee kupata habari nzuri au hali ya hewa kuwa nzuri ndiyo ujiambie una siku nzuri.
Bali siku nzuri inaanzia ndani yako mwenyewe, kwa fikra unazokuwa nazo na hatua unazochukua.

Chagua leo kuwa na siku njema kwa kuchimba ndani yako mpaka kuifikia chemchem ya wema.
Chagua leo kuwa na mtazamo sahihi, fikra sahihi na kuchukua hatua sahihi ambazo zitakuletea matokeo tofauti yatakayokufanya ujisikie vizuri sana.
Kila kitu kinaanza na wewe mwenyewe.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchimba ndani yako mpaka kuikuta chemchem ya wema, siku ya kutokutegemea wema kutoka nje yako.
#UnachotafutaKipoNdaniYako #UsihangaikeNaMamboYaNje #FikiriNaTendaKwaUsahihi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1