Rafiki yangu mpendwa,

Tafiti nyingi zinaonesha hakuna kipindi kibaya kwako kuweka malengo kama kipindi cha mwaka mpya.

Zile tarehe za mwanzo za mwaka ambapo kila mtu anaimba mwaka mpya mambo mapya ni wakati mbovu sana kwako kujiwekea malengo.

Kwa sababu sehemu kubwa ya malengo utakayojiwekea kipindi hicho, yanakuwa siyo malengo yako halisi, badala yake yanaathiriwa na malengo wanayoweka wengine.

Kwa kuwa umesikia mwenzako amesema atajenga nyumba au atanunua gari, na wewe unaona usiachwe nyuma, unayaweka kama malengo.

Sasa kinachoshangaza na kuumiza ni pale mwezi januari unapoisha, asilimia 90 ya walioweka malengo wanakuwa wameshayasahau malengo yao na kurudi kwenye maisha ambayo walishayazoea. Na hilo siyo la kushangaza, kwa sababu malengo hayo hayakuwa yao kabisa.

malengo 2020.jpg

Kutokana na changamoto hii, nimekuwa nashauri wanamafanikio wote kuanza mwaka mpya kabla ya wengine. Nimekuwa nashauri tuweke malengo na mipango yetu ya mwaka kabla wengine hawajaanza kufanya hivyo. Na wakati sahihi wa kufanya hivyo ni mapema kabisa kabla mwaka haujaanza, miezi miwili kabla ya mwaka kuisha.

Hali hii ya kuweka malengo na mipango kabla ya wengine, ndiyo imezalisha mwaka wetu wa mafanikio kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ambao unakuwa mwaka wa tofauti. Mwaka wa mafanikio unaanza novemba ya mwaka mmoja na kuisha oktoba ya mwaka mwingine. Mfano mwaka wa mafanikio 2018/2019 ulianza novemba 2018 na unaisha oktoba 2019. Mwaka wa mafanikio 2019/2020 utaanza novomba 2019 na kumalizika oktoba 2020.

Swali kwako rafiki yangu ni je ungependa kuendesha maisha yako kwa utofauti na wengine ili uweze kufikia mafanikio makubwa?

Kama jibu ni ndiyo basi sehemu sahihi kwako kuanzia ni kuwa na mwaka wa mafanikio ambao ni tofauti na mwaka wa kawaida.

Na mwaka wetu wa mafanikio 2019/2020 tutauanza kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 ambayo itafanyika tarehe 03/11/2019 jijini dar es salaam. Hii ni semina ambayo inawakusanya wanamafanikio, wale watu walio na kiu kubwa ya kufanikiwa na wanaojituma sana ili kuweza kupiga hatua kwenye maisha yao. Kwenye semina hii unajifunza mambo mbalimbali ya mafanikio pamoja na kupata shuhuda za wengine ambao wameweza kupiga hatua kubwa.

Kitu kikubwa cha tofauti ambacho utakipata kwenye semina ya mwaka huu 2019, utajiwekea lengo jipya la kifedha, ambalo utaliahidi kwa wote na utaenda kulifanyia kazi mwaka mzima ili tunapokutana kwenye semina ya mwaka unaofuata, uje na matokeo ya tofauti na ulivyoshiriki semina ya mwaka huu.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, utapata nafasi ya kujiwekea malengo na mipango ya mwaka 2020 na utapata nguvu ya kwenda kuanza kuifanyia kazi. Wakati wengine wanasherekea mwaka mpya, wewe unakuwa umeshakamilisha karibu robo ya malengo uliyojiwekea. Hii ndiyo faida ya kuuana mwaka mapema, unakuwa mbele ya wengine kwa kila kitu.

Rafiki, nichukue nafasi hii kukukaribisha sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, karibu tuwe pamoja, tujifunze, tuhamasike na tuondoke na hatua za kwenda kuchukua ili tuweze kupiga hatua zaidi mwaka 2020.

SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 itafanyika jijini Dar es salaam, jumapili ya tarehe 03/11/2019 kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa moja jioni. Itakuwa ni siku nzima ya kujifunza na kupata hamasa itakayokusukuma kwa mwaka mzima.

Kushiriki semina hii unapaswa kulipa ada ambayo ni tsh laki moja (100,000) ambayo itachangia ukumbi wa kushiriki semina, chai ya asubuhi, chakula cha mchana, chai ya jioni, kijitabu cha kuandika, kalamu na mengine yatakayopatikana kwenye siku ya semina.

Mwisho wa kulipa ada ili uweze kushiriki semina hii ni tarehe 31/10/2019. Imebaki wiki moja pekee kupata nafasi hii, hivyo chukua hatua sasa ili usiikose nafasi hii nzuri sana kwako.

Nina imani tutakuwa pamoja kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, ili tuweze kuuanza pamoja mwaka 2020 kabla wengine hawajauanza. Kamilisha malipo yako sasa kwa kutuma ada, tsh 100,000/= kwenda namba 0717 396 253 au 0755 953 887 na kisha kutuma majina yako kamili na ujumbe kwamba umelipia SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com