“What, then, makes a person free from hindrance and self-determining? For wealth doesn’t, neither does high-office, state or kingdom—rather, something else must be found . . . in the case of living, it is the knowledge of how to live.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 4.1.62–64

Kuiona siku hii nyingine nzuri ya leo ni bahati ya kipekee sana kwetu.
Siyo kwa akili zetu, wala kwa nguvu zetu tumepata nafasi hii.
Hivyo tunapaswa kuianza siku hii kwa shukrani, na kwenda kuitendea vyema kwa kufanya kilicho sahihi.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MAJUKUMU MAKUU MAWILI ULIYONAYO…
Epictetus anatuambia kitu pekee kinachotuweka huru kwenye maisha yetu siyo utajiri, kazi au wadhifa tulionao.
Bali kitu pekee kinachotuweka huru ni kujifunza jinsi ya kuishi vyema.
Na katika kujifunza jinsi ya kuishi vyema tuna majukumu makuu mawili.
Jukumu la kwanza ni kuwa mtu mweka, kwa kufanya yale ambayo ni sahihi kwako na kwa wengine.
Jukumu la pili ni kufanya kile unachopenda kufanya.
Hayo tu ndiyo majukumu makuu mawili ya maisha yako, mengine yote ni usumbufu kwako.

Unakuwa mwema pale unapowatendea wengine namna ambavyo ungependa na wao wakutendee wewe.
Kwa kujali maslahi ya wengine na kwenda hatua ya ziada katika kutoa thamani kubwa kwa wengine.
Kama unawaonea wengine, unawadhulumu au kuwaibia, kama hujali wengine, maisha yako hayawezi kuwa mazuri.

Unafanya kile unachopenda pale unapopata msukumo mkubwa kutoka ndani yako wa kufanya kitu hicho.
Pale unapokuwa tayari kufanya hata kaka hakuna anayekulipa.
Pale unapojituma zaidi kuliko wengine, unapokazana kuwa bora zaidi kila siku.

Kazana na majukumu haya makuu mawili kwenye maisha yako, na usiruhusu kitu kingine chochote kikusumbue au kukuvuruga.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa mwema na kufanya unachopenda.
#KuwaMtuMwema #FanyaUnachopenda #MaishaNdiyoHayaHaya

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1