“You have to respect every person, no matter how miserable or ridiculous he or she may be. You should remember that in every person lives the same spirit which lives in us.” —After ARTHUR SCHOPENHAUER
Usimdharau mtu yeyote, hata kama anaonekana ni wa hovyo kiasi gani.
Jua ndani ya kila mtu kuna nafsi kama uliyonayo wewe.
Na muhimu zaidi, ndani ya kila mtu kuna kitu fulani unachoweza kujifunza.
Na pia, kama wasemavyo, hata saa(ya mshale) mbovu huwa inasema ukweli mara mbili kwa siku, yule unayemdharau kuna siku atakuwa na manufaa kwako.
Mheshimu kila mtu kwa utu wake na mchango anaoweza kuwa nao kwako,
Haikugharimu chochote kuheshimu na haikunufaishi chochote kudharau.
Unapoimaliza siku hii, tafakari ni watu gani ambao umekuwa unawadharau kwenye maisha yako, kazi zako au biashara zako. Na angalia wale ni watu ambao wana watu wanawapenda na kuwathamini sana.
Na pia angalia jinsi ambavyo wamewahi kuwa na msaada kwako kwa namna moja au nyingine.
Ukawe na wakati mwema, na kesho iwe siku ya kutomdharau mtu yeyote.
Kocha.