Dunia inaendesha na kitu kimoja, hisia.
Na hii ni kwa sababu sisi binadamu huwa tunafanya maamuzi yetu yote kwa hisia kwanza na kisha kuyahalalisha kwa fikra.
Watu huwa wanatumia fedha zao kwenye vitu ambavyo vinawafanya wajisikie vizuri. Na kule ambapo fedha inapoenda, ndipo nguvu na mamlaka yalipo.
Sasa kwa kuwa watu wanafanya maamuzi yao ya kifedha kwa hisia, unaweza kupata fedha zaidi kama utaweza kugusa hisia za wengi zaidi.
Wasanii na wanamichezo maarufu wanalipwa zaidi kwa sababu kitu pekee wanachokifanya ni kuibua hisia zetu zaidi kupitia sanaa na michezo yao. Hakuna kingine unachokipata kutoka kwenye sanaa au mchezo unaoupenda bali hisia zako kuwa juu na kujisikia vizuri.
Hata vitu vingine unavyonunua, hasa vile unavyokutana navyo na kununua, ambavyo hukuwa na mpango wa kununua, kilichokufanya ununue ni kwa sababu ulijisikia vizuri kufanya hivyo. Umekutana na muuzaji anayeweza kukufanya ujisikie vizuri, ukajisikia vizuri na ukatoa fedha zako, unajikuta umenunua kitu ambacho huna matumizi makubwa nacho.
Jambo hili muhimu ambalo tumejifunza leo, kuhusu nguvu ya hisia, tunaweza kulitumia kwa pande mbili.
Upande wa kwanza ni kulinda fedha zetu, hapa unaepuka wale waliojifunza kuibua hisia za watu ili wanunue wasiweze kuibua hisia zako na kukuuzia usichotaka. Japo ni vigumu kudhibiti hisia, lakini unapojua mapema kwamba mtu anaibua hisia zako makusudi ili ununue, unaweza kuondoka haraka kabla hajafikia hisia zako.
Upande wa pili ni kupata fedha zaidi, kwa kuibua hisia za wengine na kisha kusukumwa kuchukua hatua fulani inayokunufaisha. Kama ni kitu unauza basi unamfanya mtu ajisikie vizuri kuwa na kitu hicho na hisia zake zitamsukuma anunue kile unachouza.
Kadiri unavyoweza kushawishi na kuibua hisia za watu wengi, ndivyo unavyoweza kupata fedha zaidi na hata nguvu na mamlaka.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ahsante sana kocha.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asante sana kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike