“Living doesn’t cost much, but showing off does.” – Jeffrey D. Sachs
Maisha ya kawaida hayana gharama kubwa,
Mtu yeyote anaweza kumudu gharama za msingi kabisa za maisha.
Kinachotutesa ni maigizo, kutaka kuiga wengine na kuonekana na wewe upo.
Hapo ndipo unapojikuta kwenye madeni mazito, kwa sababu tu unataka na wewe uonekane.
Haimaanishi usinunue vitu vizuri unavyotaka,
Na wala hakuna ubaya wowote kutaka kuonekana.
Ubaya ni pale unapojitesa na kusema maisha ni magumu, kumbe kinachokutesa ni maonesho na maigizo yako.
Uwe na usiku mwema, usiku wa kutafakari jinsi unavyoweza kuwa huru na kuishi maisha yanayoendana na kipato chako ili usijitese kwa maigizo na maonesho.
Kocha.
Sasa hivi wengi wanaishi kwa maonyesho ,
Kuliko kuishi uhalisi wake ina wagharimu maiaha yao hasa vijana Asante Sana kocha nitaishi maisha yangu ya uhalisi sio maonyesho
LikeLike
Vizuri Mary.
LikeLike