Basi ongeza kasi yako kwenye kuyaishi maisha yako.

Lakini kuongeza kasi ya maisha kabla hujajua nini unataka kwenye maisha yako ni hatari, ni sawa na kuongeza mwendo huku ukiwa hujui wapi unakwenda, unazidi kujipoteza.

Unaongeza kasi ya maisha kwa kuyanya yale ambayo unataka kufanya, kwa kuanza sasa na siyo kusubiri.

Biashara ambayo umekuwa unajiambia unataka kuifanya, wakati sahihi wa kuanza kuifanya ni sasa. Siyo kusubiri mpaka kesho au kusubiri mpaka uwe tayari, bali kwa kuanza sasa.

Kitabu ambacho umekuwa unajiambia unataka kuandika, wakati sahihi wa kukiandika ni sasa. Huna tena haja ya kuendelea kusubiri, huna unachosubiri, unapaswa kuanza kuandika sasa.

Usiache nafasi yoyote ikupite, ifanyie kazi sasa, kama ndiyo kitu unachokitaka kweli.

Unaposema maisha ni mafupi, basi maanisha kweli, usiendelee kuyapoteza maisha yako kwa kuhangaika na yasiyo muhimu huku ukiahirisha yale muhimu. Ongeza kasi ya maisha yako, kwa kuondoa yasiyo muhimu na kukazana na yale muhimu.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha