Kuna sheria ambazo hazijaandikwa popote na wala hulazimiki kuzifuata, lakini kwa kuwa unaishi kwenye jamii ambayo kila mtu anazifuata, basi unajikuta na wewe ukizifuata.
Lakini sheria hizo zinakubana, zinakuzuia usifanikiwe.
Mfano sheria iliyozoeleka kwamba lazima ufanye kazi masaa nane kwa siku, siku tano za wiki, kwamba mwisho wa wiki ni siku za mapumziko na unapaswa kupumzika. Karibu kila mtu anafuata sheria kama hiyo, japo hakuna anayelazimishwa kuendesha maisha yake hivyo.
Ukiwaangalia wale waliofanikiwa sana, utaona kabisa wamejitengenezea sheria zao wenyewe na kuziishi. Wameachana na sheria za kwenye jamii ambazo zinawabana wasifanikiwe.
Kwa kuachana na sheria za kijamii na kuchagua kufuata sheria zao wenyewe, huwa wanasemwa vibaya na wengine, huwa wanashambuliwa, kukosolewa na kukatishwa tamaa, lakini hayo yote hayawatetereshi kwa sababu wanajua wanachotaka na jinsi ya kukifikia.
Huwezi kupata mafanikio makubwa kwa kuishi kama ambavyo kila mtu anaishi, huwezi kuwa huru na maisha yako kama unafuta sheria ambazo kila mtu anataka ufuate.
Jiwekee sheria zako binafsi, sheria zitakazokufikisha kule unakotaka kufika na kisha zifuate hizo. Ukifuata sheria nyingine nje ya hizo utakutana na vikwazo vinavyokuzuia usifanikiwe.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Wakati nasoma hapa nikapata wazo moja,ikiwa nimeajiriwa serikalini na Nina mapumziko week end Je siwezi tumia siku hizo kujitolea kufanya kazi kwenye kile nilichopanga kukifanya nje ya ajira? Ili nitakapokianza niwe na uzoefu?pengine ni kuwa na CAFETERIA basi niwe naenda Fanya kazi kwenye cafeteria bila malipo ila najifunza, hili limenitafakarisha sana, Asante kocha.
LikeLike
Wazo zuri sana hilo,
Lifanyie kazi.
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha , nitaweka sheria zangu zitakazoendesha maisha yangu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kweli tupu kocha. Ahsante, kila la kheri.
LikeLike