Set aside a certain number of days, during which you shall be content with the scantiest and cheapest fare, with course and rough dress, saying to yourself the while: “Is this the condition that I feared?” —SENECA
Kuna vitu vingi sana unavyohofia kwenye maisha yako.
Kwa kuhofia vitu hivyo, unashindwa kuyafurahia maisha yako.
Ipo njia rahisi ya kuondokana na hofu hiyo ili uweze kuyafurahia maisha yako.
Njia hiyo ni kutenga siku za majaribio,
Siku za kujaribu kile ambacho unahofia.
Seneca anatuambia tutenge siku ambazo tutaishi kwa hali ya chini kabisa,
Kula chakula cha chini, kuvaa mavazi ya chini kabisa kisha kujiuliza hayo ndiyo unayohofia?
Kama umezoea kulala kwenye kitanda, kwenye siku ya majaribio lala chini.
Kama umezoea kutumia usafiri wako, kwenye siku ya majaribio tumia usafiri wa umma au tembea kwa miguu.
Siku hizi za majaribio zinakufanya ujue kwamba hata ukipoteza kila ulichonacho, maisha yako yataendelea.
Hivyo hofu ya kupoteza ulivyonavyo haikusumbui, kwa sababu unajua siyo mwisho wa dunia.
Siku hizi za majaribio pia zinatufundisha kujali vitu wakati tunavyo.
Unaweza kuwa umeshazoea kulala kwenye kitanda chenye godoro zuri na kuona ni kitu cha kawaida kwako.
Lakini siku utakayolala chini, utauona umuhimu wa kitanda, na utakapolala tena kwenye kitanda, utakithamini sana.
Tenga siku za majaribio, utaiondoa hofu na kujikumbusha thamani ya vitu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania