“In Zen they say: If something is boring after two minutes, try it for four. If still boring, try it for eight, sixteen, thirty-two, and so on. Eventually one discovers that it’s not boring at all but very interesting.” – John Cage
Kama kuna kitu muhimu kwako kufanya, lakini hujisikii kukifanya, anza kukifanya kwa muda mfupi, kisha zidisha muda huo.
Jiambie utafanya kwa dakika 2, ikiwa bado hujisikii, fanya kwa dakika 4, kama bado fanya kwa dakika 8.
Endelea kuzidisha muda mara mbili mpaka pale utakapofikia hatua ya kujisikia na kufurahia kitu hicho.
Umekuwa fundi wa kuahirisha mambo kwa sababu pale tu unapokuwa hujisikii kufanya kitu, unaacha mara moja kukifanya.
Usichojua ni kwamba kujisikia kunatengenezwa na kufanya.
Kwa maneno mengine, usisubiri mpaka upate hamasa ndiyo ufanye kitu, bali anza kufanya kitu na utatengeneza hamasa.
Usiache kufanya kitu kwa sababu hujisikii kukifanya, bali endelea kukifanya na utajisikia kukifanya.
Tatizo kubwa ni kwamba una njia nyingi sana za kutoroka, umejiambia unataka kusoma kitabu au kuandika, lakini hujisikii kufanya hivyo, unatorokea kwenye simu yako, unaingia mtandaoni na hapo huwezi tena kurudi kwenye kile ulichopanga.
Usikimbilie kutoroka, tumia kanuni hii ya kuzidisha muda wa kifanya kitu na utaona jinsi unavyoweza kufanya makubwa.
Leo nenda katenge muda wa kufanya yale muhimu, na anza kwa muda mfupi huku ukiendelea kuzidisha muda huo mpaka unalize ulichopanga.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania