“Familiarity breeds contempt, while rarity wins admiration.” – Apuleius

Hakuna mtu anayeweza kukudharau bila ya wewe kumruhusu kufanya hivyo.
Na njia ambayp umekuwa unawaruhusu watu wa kudharau ni kupitia mazoea.
Kadiri watu wanavyozoea mtu au kitu, ndivyo wanavyokidharau.
Kabla watu hawajazoea mtu au kitu, wanaheshimu.
Wakishazoea wanadharau, wanachukulia poa.
Kabla watu hawajakujua wanakuheshimu,
Wakishajua kila kitu kuhusu wewe wanakudharau na kukuchukulia poa.
Watu wakijua muda wako haupatikani kirahisi wanauthamini,
Wakijua unapatikana kila wakati wanadharau muda unaowapa.

Ni kanuni ya asili, na wala siyo kwamba watu wanafanya kwa makusudi.
Kwa asili, kitu chochote kinachopatikana kwa wingi, thamani yake huwa ni ndogo.
Mfano dhahabu na chuma vyote ni madini,
Inatumia gharama kubwa kufua chuma kuliko dhahabu,
Chuma kina matumizi mengi kuliko dhahabu.
Lakini thamani ya dhahabu ni kubwa kuliko ya chuma, kwa sababu chuma inapatikana kwa wingi na urahisi kuliko dhahabu.

Kuwa dhahabu,
Weka mipaka baina yako na wengine,
Usiruhusu mtu yeyote kukujua kupita kiasi,
Usiwe mtu wa kuanika kila jambo kuhusu wewe,
Uthamini sana muda wako, usiruhusu upotee bure,
Na kazi zako zisiwe za kawaida, bali za kipekee na utofauti.
Kwa njia hizi, utaondoa mazoea na kujenga heshima.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania