Rafiki yangu mpendwa,

Siyo siri kwamba nyakati tunazopitia sasa ni ngumu.

Ili kuvuka nyakati hizi, unahitaji kuwa na msingi imara sana wa maisha yako ambao hautetereshwi na kitu chochote.

Na kwa bahati mbaya sana, hicho ndiyo kitu ambacho wengi wamekosa. Hivyo inakuwa rahisi sana kwao kushawishiwa na kundi kubwa la watu au vyombo vya habari ambavyo vinavumisha zaidi habari hasi kuliko chanya.

Hapa ndipo mimi rafiki yako ninapokuja kwenye maisha yako, nikikushirikisha maarifa sahihi ambayo yatakupa msingi sahihi utakaokuwezesha kuvuka chochote unachopitia.

Kuna kitabu kimoja nakushauri sana ukisome kama bado hujafanya hivyo. Na kama ulishakisoma huko nyuma, rudia tena kukisoma sasa. Ni kitabu chenye maarifa ambayo yanakujenga kujiamini na kuwa na msingi sahihi wa kuyaishi mafanikio yako.

Kitabu hicho kinaitwa MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.

Kama jina la kitabu linavyoeleza, ni kweli kwamba wewe ni mshindi. Lakini ushindi wako hautakuja kirahisi, lazima uishi misingi fulani ambayo itakufikisha kwenye ushindi. Misingi hiyo ndiyo unakwenda kujifunza kwenye kitabu hicho.

Kwenye kitabu hiki, kuna kiapo cha ushindi ambacho unapaswa kujipa wewe mwenyewe. Kwenye kiapo hicho unajiahidi kuyaishi maisha mapya ya ushindi na yale utakayosimamia ili kuweza kuishi maisha hayo.

Hakuna aliyesoma kitabu hiki na akabaki kama alivyo, shuhuda za wengi zinaonesha jinsi kitabu hiki kimekuwa na manufaa kwao.

WhatsApp Image 2020-04-08 at 07.21.24.jpeg

Huu ni moja ya ushuhuda wa wale walionufaika na kitabu hiki;

Hicho (MIMI NI MSHINDI) ni moja ya vitabu nilivyosoma na kujifunza mambo mengi, ukweli kujenga msingi bora na imara sio kazi ndogo wala kusema utafanya kwa muda mfupi, lazima kuendelea kujifunza huku ukiwa na mtu makini, mfano mdogo. Mara nyingi Kocha umekuwa ukisisitiza watu kuwa na biashara hata Kama ni kidogo, kutenga mafungu mbalimbali ya kuwekeza, kujilipa kuweka akiba, dharura n.k, hiyo sio kazi rahisi kwa mtu anayeanza, Ila ukianza na ikawa utaratibu wako ndio utajua umuhimu wake. Binafsi nakubali kuendelea kujifunza kila siku, kuweka kazi mbele, nia, mipango na malengo huku nikiwa nayatekeleza, naona nilipo na najua ninakokwenda safari hii sio nyepesi ila najua iwe kufa au kupona, ije mvua au jua, mimi sio wa kulalamika au kulaumu, bali jukumu langu kuu ni kutatua hizo changamoto na kuvuka vikwazo na kusonga mbele, mafanikio kwangu nikiwa hai ni lazima. – Beatus E.

Rafiki, ninachotaka ni wewe pia uweze kusema hivyo, uweze kujiahidi ushindi, ujitoe kwa kila namna kupiga hatua licha ya mambo kuwa magumu. Na hilo ni jambo ambalo linawezekana kwako ukiwa na misingi sahihi. Na misingi sahihi unaipata kwenye kitabu cha MIMI NI MSHINDI.

Kitabu hiki ni nakala tete (softcopy) na kinatumwa kwa email. Bei ya kitabu hiki kwa kawaida ni tsh elfu 10 (10,000/=), lakini kama utakilipia leo, utakipata kwa bei ya zawadi ambayo ni tsh elfu 7 (7,000/=)

Kupata kitabu hiki, tuma tsh elfu 7 (7,000/=) kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na maelezo umelipia kitabu cha MIMI NI MSHINDI na utatumiwa kitabu hicho.

Umezaliwa kushinda, nenda kaishi ushindi wako leo na kila siku kwa kuwa na mwongozo sahihi unaopatikana kwenye kitabu cha MIMI NI MSHINDI.

Zawadi ya vitabu nane vya mafanikio.

Rafiki, nikukumbushe pia kwamba zawadi ya vitabu nane nilivyotoa inaendelea na karibu itafika ukingoni.

Kwenye zawadi hii, unapata vitabu nane nilivyoandika, katika mfumo wa nakala tete kwa kulipa nusu ya bei pale unapochukua vitabu vyote.

Vitabu hivyo na bei zake za zawadi ni kama ifuatavyo;

  1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, bei ya zawadi elfu 3.
  2. JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG, bei ya zawadi elfu 7.
  3. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA, bei ya zawadi elfu 3.
  4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, bei ya zawadi elfu 7.
  5. BIASHARA NDANI YA AJIRA, TOLEO LA KWANZA, bei ya zawadi elfu 7.
  6. MIMI NI MSHINDI, AHADI YANGU NA NAFSI YANGU, bei ya zawadi elfu 7.
  7. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING), bei ya zawadi elfu 3.
  8. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, bei ya zawadi elfu 3.

Ukichukua vitabu vyote nane kwa pamoja, unalipa tsh elfu 30 badala ya elfu 40 kama utachukua kimoja kimoja kwa bei ya zawadi.

Karibu sana upate zawadi hii, tuma fedha kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu au vitabu ulivyolipia kisha utatumiwa kwenye email yako.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania