“For a person who leads a spiritual life, self-sacrifice brings a bliss that far transcends the pleasure of a person who lives by the self-indulgent satisfaction of his animal passions.” – Leo Tolstoy
Kwa mtu anayeishi maisha ya kiroho, kujinyima kunamfanya awe bora na kujisikia vizuri kuliko yule ambaye anatimiza kila aina ya tamaa aliyonayo.
Kila tamaa unayoishinda inakufanya kuwa bora zaidi ys ulivyokuwa kabla.
Huku wale wanaotimiza kila aina ya tamaa wakizidi kuwa hovyo kwa kila tamaa wanayootimiza.
Kuishinda tamaa kunakuweka huru,
Kuitekeleza tamaa kunakufanya kuwa mtumwa zaidi.
Kila tamaa unayoishinda unajenga nguvu zaidi ndani yako kwamba unaweza kufanya makubwa na wewe ndiye mwamuzi wa mwisho wa maisha yako.
Kila tamaa unayoitekeleza inakufanya kuwa dhaifu zaidi na kuwa tegemezi kwenye yamaa hiyo, huku ukijiona huna maamuzi yoyote kwenye maisha yako, unaburuzwa tu na tamaa zako.
Nenda kashinde kile tamaa leo, anza kwa kujinyima vitu vidogo vidogo ambavyo umeshavizoea.
Kila unapojiambia unataka kuingia mtandaoni, jikataze kwa muda.
Kila unapojiambia unataka kula kitu kitamu au kinachosisimua, jikataze kwa muda.
Kujinyima vile ambavyo umeshazoea kuwa navyo au kufanya kila mara, ni hatua muhimu ya kushinda tamaa zako na kuwa imara zaidi kiroho.
Ishinde tamaa ili uwe bora zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania