“Most of our spending is done to forward our efforts to look like others.” —RALPH WALDO EMERSON

Sehemu kubwa ya matumizi yanayokusumbua sana siyo yake ya msingi,
Bali ni yale matumizi ya anasa,
Matumizi ambayo lengo lake ni kufanana na wengine, kukazana usipitwe na wengine.
Sisi binadamu huwa hatupendi kuwa nje ya kundi,
Hivyo kile wanachokifanya wengine, ndiyo tunakifanya pia.
Tatizo kubwa linakuja pale kitu hicho kinapokuwa nje ya uwezo wetu,
Tunajisukuma na kujiumiza ili tu kupata kile ambacho wengine wanacho.
Tunakopa au kuteseka kwa kazi za ziada, ila lengo ni kupata kile walichonacho wengine.

Kama bado maisha yako yanaendeshwa kwa kuwaangalia wengine, hujawa huru kwenye maisha.
Ni lazima uwe tayari kuishi maisha yako na kuwaacha wengine waishi maisha yao.
Kama jambo siyo muhimu kwako usilifanye, hata kama kila mtu anafanya.
Muda na fedha ulizonazo vina ukomo, hivyo vitumie kwa umakini mkubwa.
Kama kitu siyo muhimu kwako usifanye, hata kama kila mtu anafanya.
Huo ndiyo uhuru kamili wa maisha yako, kuishi kwa vigezo vyako na siyo vya wengine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania