“You should always be truthful, especially with a child. You should always do what you have promised him, otherwise you will teach him to lie.” —After the TALMUD

Watoto huwa wanajifunza kudanganya kupitia wazazi na walezi wao.
Wanaangalia sana kile ambacho mtu anaahidi na jinsi anavyokitimiza.
Hilo wanalielewa na kulikariri kuliko kile ambacho mtu anasema.
Yaani watoto wanaelewa na kukariri jinsi tunavyofanya, kuliko tunavyosema.
Hivyo kama kuna tabia tunataka kuijenga kwa watoto, lazima tuanze kuifanya sisi wenyewe.

Ni rahisi kuona kwamba kuwadanganya watoto siyo shida,
Hasa pale unapowataka wafanye kitu fulani.
Lakini watoto hao hujifunza na kukariri,
Na baadaye kuiga kile ambacho tumekifanya pia.
Halafu tunakuja kulalamika kwamba watoto hawasikii kile wanachoambiwa.
Ni kweli hawasikii, kwa sababu matendo yako yanateka zaidi macho yao kuliko maneno yako yanavyoteka masikio yao.

Kuwa mtu wa kusema ukweli mara zote,
Na kuwa makini zaidi na ahadi zako kwa watoto,
Maana huwa hawasahau na hujifunza kupitia unachofanya na siyo unachosema.
Na hata kwenye mahusiano yetu mengine,
Tunapaswa kuyajenga kwenye msingi wa ukweli.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
Www.t.me/somavitabutanzania