“Fear nobody and nothing. That which is the most precious matter in you can be damaged by no one and by nothing.” – Leo Tolstoy
Watu wanapotaka kukutawala au kunufaika na wewe, huwa wanaanza na kitu kimoja, hofu.
Wanakufanya uwahofie, uone kwamba wanao uwezo wa kuyaharibu maisha yako au kuchukua chochote ulichonacho.
Ukishaingiwa na hofu juu ya yeyote au chochote, huwezi tena kuwa huru.
Hofu inakufanya uone wengine wana nguvu juu yako.
Hofu inakuaminisha kwamba bila ya watu hao wewe huwezi chochote.
Hivyo unakuwa umewapa watu hao silaha nzuri ya kukumaliza.
Ukitaka kuwa huru na maisha yako, usimhofie mtu yeyote wala kitu chochote.
Kuwa jasiri na jiamini wewe mwenyewe.
Ukijua ya kwamba kile kitu cha thamani zaidi kilichopo ndani yako, hakiwezi kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote.
Hakuna awezaye kufikia roho yako bila ya wewe kumruhusu,
Na roho yako ndiyo kitu cha muhimu zaidi kwako,
Ndiyo kitu kinakufanya wewe kuwa mtu.
Jukumu lako kubwa la kila siku ni kushinda kila aina ya hofu.
Kujua kwamba hakuna hofu yenye nguvu dhidi yako, mpaka pale wewe unapoipa hofu.
Na wale wanaokujengea hofu, ni kwa sababu hawana nguvu ya kuyaharibu maisha yako, hivyo wanakutega uyaharibu mwenyewe.
Ukishakuwa na roho yako, huna chochote chs kupoteza.
Kwa kuwa hakuna ulichokuja nacho,
Na hakuna utakachoondoka nacho,
Hivyo mtu anapokutishia kukunyima au kukunyang’anya vitu ambavyo hukuzaliwa navyo, mpuuze.
Mtu huyo hana nguvu juu yako, ila anataka kukujengea hofu ili akutawale.
Unapokuwa tayari kupoteza chochpte ulichonacho, hakuna yeyote anayeweza kukutishia au kukutawala.
Hivyo kama unataka uhuru kamili wa maisha yako, usimwogope mtu yeyote wala kitu chochote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante kocha , kweli sikuja duniani na hakuna nitakachoondoka nacho hapa duniani, nitaendelea kujiamini Mimi mwenyewe
LikeLike
Karibu James
LikeLike