Kwenye ujenzi huwa kuna kauli maarufu kwamba hupaswi kuchezea au kupoteza ‘matirio’, yaani rasilimali zote zinazotumika kwenye ujenzi. Usipokuwa na mipangilio mizuri kwenye ujenzi, unaweza kukuta umetumia vibaya rasilimali na hujafikia lengo.
Kauli hii inaweza kutusaidia sana kwenye maisha na safari yetu ya mafanikio. Maisha huwa yanakupa rasilimali mbalimbali, lakini wewe umekuwa unazichezea au kuzipoteza na hivyo kushindwa kuzitumia vizuri kwa manufaa yako.
Kila kinachokuja kwenye maisha yako, kiwe kizuri au kibaya, unakipenda au hukipendi, jua ni rasilimali muhimu ya kukuwezesha ufanikiwe zaidi.
Jua likiwaka, palilia vizuri bustani yako.
Mvua ikinyesha, kinga maji na nyeshea bustani yako.
Kinyesi kikikuangukia, kigeuze kuwa mbolea kwenye bustani yako.
Watu wakikupiga mawe, yakusanye na jenga ukingo wa bustani yako.
Kila kitu ni rasilimali, ni mtazamo wako kwenye kitu hicho na jinsi unavyokitumia.
Kila unachokutana nacho kwenye maisha, jiambie haya ni matirio, je naweza kuyatumiaje kwa manufaa yangu? Na hapo utaona njia bora za kutumia kila kinachokuja kwako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ahsante sana kocha, napaswa kutumia vizuri matirio yoyote yanayokuja kwenye maisha yangu kwa ajili ya kuyajenga mafanikio yangu.
LikeLike
Ahsante sana kocha, napaswa kutumia vizuri matirio yoyote yanayokuja kwenye maisha yangu kwa ajili ya kuyajenga mafanikio yangu. Kila la kheri.
LikeLike
Vizuri Tumaini.
LikeLike
Asante sana kocha hili ni jambo la msingi sana kulifahamu, Kila kitu ni rasilimali muhimu kwetu tatizo hatujuwi kuzitumia rasilimali hizo.
LikeLike
Hakika, tukiwa na mtazamo huu wa rasilimali, tutatumia vitu vizuri.
LikeLike
Ukurasa huu umenigusa Sana. Tinahitaji kuwa na mtazamo Chanya kwenye maisha kwa kila kinachotokea.
Vita pia ni fursa kwa wengine wanaouza silaha, chakula, Mavazi nk.
Kila Changamoto ni fursa
Kila kinachotokea maishani kwangu kina matumizi Chanya kwenye maisha yangu.
LikeLike
Hakika
LikeLike