“You must do the thing you cannot do.” – Eleanor Roosevelt

Kama kuna kitu unataka kufanya,
Lakini unajiambia huwezi kufanya,
Basi kifanye kiwe lazima kwako kufanya.
Huwa tunakua pale tunapofanya vitu ambavyo hatuwezi kufanya.
Tunapata mafanikio pale tunapofanya vitu vya tofauti,
Kuendelea kufanya kile ulichozoea,
Utaendelea kupata matokeo ambayo umekuwa unapata,
Ambayo hayawezi kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.

Jiwekee sheria hii mpya ambayo itakusaidia sana,
Kama kuna kitu unapaswa kufanya lakini huwezi kufanya, basi hicho ni lazima kwako kufanya.
Kama kuna kitu umepanga kufanya lakini unahofia kufanya, kifanye kuwa lazima kukifanya.
Ni rahisi kukimbia vitu vigumu na tunavyohofia,
Lakini ndiyo vitu pekee vinavyotusukuma kukua zaidi ns kupiga hatua za tofauti.

Kila mara kazana kufanya vitu vilivyo nje ya mazoea yako,
Jaribu vitu vipya kila wakati,
Panga kufanya makubwa zaidi ya ulivyozoea,
Tumia njia za tofauti na ulivyozoea,
Fanya kile unachohofia.

Kila unachofanya kwenye maisha yako, kuna tabia unaijenga na kuiimarisha.
Ukiwa ni mtu wa kikimbia mambo magumu na unayohofia, hiyo ndiyo tabia utakayojijengea na hutaweza kufanya makubwa.
Lakini ukiwa mtu wa kukabiliana na kila linalokuja mbele yako,
Una nafasi ya kufanya makubwa sana.

Kuanzia leo, unapokuwa na kitu cha kufanya na ukajiambia huwezi, hapo hapo jiambie ni lazima ukifanye.
Kuna wengi ambao wameweza kufanya,
Hawakuzaliwa wakijua kufanya.
Hivyo hata wewe utaweza kufanya iwapo utaamua kweli.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania