Rafiki yangu mpendwa,

Wakati naanza safari ya kujifunza misingi sahihi ya kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha, nilikutana na njia rahisi ya kusoma vitabu vingi ambayo ilikuwa ni kusikiliza vitabu vilivyosomwa (AUDIO BOOKS).

Nakumbuka audio za kwanza kabisa kusikiliza zilikuwa za waandishi wawili ambao nilijifunza mengi sana kwao, wa kwanza alikuwa Brian Tracy ambaye nilijifunza siri 21 za karibu kila kitu, mfano siri 21 za kuwa milionea, siri 21 za kulipwa zaidi, siri 21 za kupata muda zaidi n.k.

Mwandishi wa pili niliyejifunza mengi sana kwake kupitia kusikiliza audio alikuwa Zig Zigler ambaye pamoja na mengi niliyojifunza kwake, nilijifunza falsafa sahihi ya maisha ya mafanikio ambayo tangu kipindi hicho nimekuwa naiishi na naona matokeo yake makubwa.

Kwa kuona matokeo ya falsafa hiyo kwenye hatua ndogo kumekuwa kunanipa uhakika wa kuweza kufikia lengo lolote kubwa nililonalo.

Hivyo katika lengo moja kubwa kati ya mawili makubwa niliyonayo, yaani lengo la kuwa bilionea, nina uhakika wa kulifikia kwa sababu ninachofanya ni kuiishi falsafa niliyojifunza kutoka kwa Zig Zigler.

Leo nakwenda kukushirikisha Falsafa hiyo na kukukaribisha twende pamoja ili wote tuweze kunufaika kwa kupata kile tunachotaka.

Kabla sijakushirikisha falsafa hiyo, nikupe kwanza hadithi ambayo nilijifunza kwa Zigler na ikanisaidia sana kuelewa falsafa hiyo.

Hadithi yenyewe inakwenda hivi;

Bwana mmoja alifariki na alipofika ahera alipewa nafasi ya kwenda peponi au motoni. Kwa kuwa hakuwa na uhakika aliomba atembezwe sehemu zote mbili halafu atachagua ni wapi pa kwenda. Alipelekwa motoni akakuta watu wamekaa kwenye meza ya duara mbele yao kuna vyakula vizuri sana tunavyovipenda duniani. Ila hakuna aliyekuwa anakula na wote walikuwa wamekonda na hawana furaha kwa njaa kubwa waliyokuwa nayo.

Baada ya pale alipelekwa peponi na alikuta watu wamekaa vile vile kwenye meza ya duara na vyakula vizuri mbele yao. Ila kikubwa alichoona hapa watu walikuwa wanakula kwa furaha na walikuwa na afya njema.

Baada ya ziara zile yule bwana alichanganyikiwa, aliuliza ni kipi kinawafanya walioko peponi kula kwa furaha wakati walioko motoni wanakufa kwa njaa na vyakula viko mbele yao?

Aliyekuwa anamtembeza alimpa jibu moja; hukuangalia vizuri, watu wote waliko peponi na waliko motoni wana umma wenye urefu wa mita moja, ni vigumu sana kujilisha mwenyewe kwa umma mrefu kiasi hicho. Walioko peponi waliweza kula kwa sababu kila mmoja aliamua kumlisha aliyeko upande wa pili wa meza (kumbuka wamekaa meza ya duara) hivyo kila aliyelisha naye alilishwa. Kule motoni kila mtu alishindwa kula kwa sababu alikuwa anafikiria kujilisha yeye kwanza, kitu ambacho hakiwezekani kutokana na ukubwa wa umma waliokuwa wanatumia. Hivyo walikuwa wanakufa njaa huku chakula kikiwa mbele yao kwa sababu ya ubinafsi.

Unajifunza nini kwenye mfano huu?

Hapa ndipo Zigler anapokuja na falsafa yake maarufu ambayo kwa Kiingereza inasema; You Can Have Everything In Life You Want, If You Will Just Help Enough Other People Get What They Want.

Kwa Kiswahili unaweza kusema; unaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako kama utawasaidia wengi zaidi kupata kile wanachotaka.

Hiyo ndiyo falsafa kuu ya mafanikio niliyojifunza kutoka kwa Zig Zigler na nimekuwa naiishi kila siku.

Kwa chochote kile ambacho mimi nataka, nimekuwa najisahau kwanza mwenyewe na kuangalia nani anataka kitu kama hicho, kisha nimsaidie kukipata na hapo ndipo mimi nitapata ninachotaka.

Kwa lengo langu kubwa la kuwa bilionea, sijiangalii mwenyewe nawezaje kuwa bilionea, bali naangalia nawezaje kuwasaidia watu wengi zaidi kuwa mabilionea. Kwa sababu najua nikiweza kufanya hivyo, hakuna kinachoweza kunizuia mimi nisiwe bilionea.

Ndiyo maana nakuambia lengo langu kubwa ni kukusaidia wewe uweze kuwa tajiri. Kwa sababu wewe ukiwa tajiri, lazima na mimi nitakuwa tajiri.

Lakini siwezi kukusaidia wewe kuwa tajiri kama wewe mwenyewe hujawa tayari. Hivyo kitu kimoja kikubwa ninachokuomba ni uwe tayari kujitoa kweli kufikia utajiri, kisha karibu tusafiri pamoja.

Safari hii siyo rahisi, ina vikwazo vya kila aina, ina tamaa nyingi za kukuondoa kwenye njia sahihi, lakini ni safari inayowezekana pale unapoamua.

Karibu tusafiri pamoja kwenye lengo hili kubwa.

Rafiki yangu mpendwa, huwa napenda kutumia neno TUKO PAMOJA kwa sababu namaanisha kweli kwamba kwa yule ambaye atakwenda pamoja na mimi atafikia mafanikio makubwa sana kwenye maisha yake. Kwa yeyote ambaye atajifunza yale ninayojifunza na akayatumia kwenye maisha yake nina uhakika mkubwa atafanikiwa. Ila kama hutatumia yale unayojifunza na kubadili maisha yako tutakuwa pamoja kwa maneno lakini mwisho wa siku utabaki nyuma na kuanza kulalamika haiwezekani kufikia malengo makubwa.

Hivyo niendelee kukaribisha wale ambao wanataka kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao, basi wakaribie tuwe pamoja na twende pamoja kwenye safari hii.

Njia nzuri ya kuwa pamoja na mimi kwenye hii safari ni kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Kutokana na mafunzo ninayotoa kuafikia maelfu ya watu, ninakuwa sina muda wa kuweza kumfikia na kumfuatilia kila mtu kwa karibu. Hivyo kuna nafasi chache za wale ambao wanapenda tuwe karibu na kupiga hatua kubwa. Nafasi hiyo ni kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa kwenye KISIMA, unapata nafasi ya kujifunza mengi sana, kupata mwongozo sahihi wa mafanikio na hata kufuatiliwa kwa karibu. KISIMA CHA MAARIFA kinakupa jamii ya tofauti, jamii inayokupa moyo wa kufanikiwa hata kama unapitia magumu.

Rafiki yangu mpendwa, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi jua unajichelewesha sana kufikia mafanikio makubwa. Unajiweka kwenye hatari ya kuendelea kuhangaika na fursa mpya kila wakati na kujichosha huku ukiwa huna matokeo makubwa unayozalisha.

Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii, ili upate nafasi ya kuishi kwa falsafa bora kabisa za mafanikio, ambazo zinakupa uhakika wa kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania